Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa mkataba wa mauziano ya kiwanja kati ya aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Takukuru Godfrey Gugai, na aliyemuuzia Abubakar Hamis uliandikwa Sh.milioni 60 lakini walipewa Sh.milioni 80 ili wapate ahuweni ya kodi.

Hamis (46), ambae ni mkazi wa Boko, na shahidi wa 20 katika kesi utakatishaji fedha na kumiliki mali zilizozidi kipato, inayomkabili Gugai na wenzake wanne.

Akiongozwa na Wakili wa serikali kutoka (Takukuru) Awamu Mbagwa, kutoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, shahidi huyo amedai mahakamani hapo  kuwa Gugai ni jirani yake na amewahi kufanya nae biashara.

Amedai walifanya makubaliano baina ya familia ya Gugai ya kuuziana kiwanja namba 64 kilichopo kitalu C eneo la Boko Ununio Dar es Salaam, kwa Sh. milioni 80 na malipo yalifanyika kwa fedha taslimu ambapo mwanasheria wake alienda kuandaa mkataba na walipofika nyumbani kwake jioni aliwapa na kuusoma kisha akawakabidhi fedha.

Shahidi ameendelea kudai kuwa mkataba huo uliandikwa Sh.milioni 60 tofauti na makubaliano lakini walikabidhiwa fedha taslimu Sh.milioni 80 na uliandikwa hivyo ili kuweza kupata ahuweni ya kodi.

Baada ya maelezo hayo, shahidi huyo aliiomba Mahakama kupokea mkataba wa mauziano ya kiwanja kama kielelezo baada ya kuutambua kwa majina na saini lakini upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Semi Malimi ulipinga kupokelewa kwa mkataba huo wakidai kuwa ni nakala na sio nyaraka halisi ya mkataba.

Alidai nakala yoyote inayotolewa mahakamani lazima iwe halisi kwa mujibu wa sheria kifungu 67 (1) na kama ni nakala yapo mazingira yanayoruhusu ipokelewe.Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 11, mwaka huu atakopotoa uwamuzi kama kielelezo hicho kipokelewe au la.

Gugai na mwenzake watatu wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo, makosa 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai.Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo, ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.

Kwa mara ya kwanza washitakiwa hao walifikishwa Mahakamani Novemba 16 mwa 2017 ambapo walinyimwa dhamana kutokana na shtaka la utakatishaji kutokuwa na dhamana.Katika kesi ya msingi, Gugai na mwenzake, wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai.


Gugai anakabiliwa na kosa la kumiliki mali kinyume na kipato chake, ambapo alitenda kosa hilo kati ya January 2005 na Decembea 2015.Inadaiwa kuwa akiwa Takukuru Dar es Salaam, Gugai alikuwa akimiliki mali za zaidi ya Sh bilioni 3.6 ambazo hazilingani na kipato chake huku akishindwa kuzitolea maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...