Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Kampuni kutoka nchini China inayojishughulisha na masuala ya Bishara Mtandaoni imetambulishwa rasmi nchini Tanzania na kwa Watanzania kwa ujumla.

Longrich Internaltional yenye miaka 33 tangu kuzinduliwa ambapo Makao Makuu yake yapo nchini China imekuja nchini kutoa fursa katika suala la Biashara ya Mtandaoni.

Akizungumza wakati wa utambulisho wa Kampuni hiyo, Afisa Tarafa wa Wilaya ya Ilala, George Anthony amesema Serikali ya Tanzania ipo kwenye mkakati wakuvutia Wawekezaji na Biashara, amesema wanaikaribisha Longrich huku akisema Serikali inaahidi kuwa bega kwa bega kuweka mazingira sahihibya kufanya biashara.

Amewaomba Longrich wasiifanye Tanzania kama Soko, ametoa wito kwa Kampuni kama hizo kuja kuwekeza Viwanda vya Uzalishaji wa bidhaa zao hapa Tanzania, kama Serikali inavyojipambanua kuwa ya Viwanda.

Kwa Upande wake, Meneja wa Longrich Tanzania, Pino Zhang amesema Longrich ni moja ya Kampuni kubwa nchini China iliyo katika 10 Bora za Kampuni zilizopo nchini humo, amesema Longrich International ina matawi Ulimwenguni kote sio Tanzania pekee, pia ina Matawi katika nchi za Ghana, Afrika Kusini, Zambia, Kenya, Rwanda na Ivory Coast.

Balozi wa Kampuni hiyo, Flora Vitalis amesema kuwa Longrich imeleta bidhaa za Mimea Asili kwa Watanzania, amesema tayari wamefungua milango kwa Watanzania wengi kujipatia bidhaa hizo zenye ubora, kama vile Taulo za Kike, Viatu.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Malkia wa Nguvu Tanzania, Grace Mpanduka ametoa wito kwa wanawake kutunza ngozi zao kwa kutumia bidhaa hizo za Mimea asilia kwani zina ubora wa hali ya juu.
Afisa Tarafa wa Wilaya ya Ilala, George Anthony (kulia) akizngungumza na waandishi wa bahari wakati wa utambulisho wa kampuni Longrich kutoka nchini China inayojishughulisha na masuala ya Bishara Mtandaoni leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Afisa Tarafa wa Wilaya ya Ilala, George Anthony (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Meneja wa Longrich Tanzania, Pino Zhang mara maada ya utambulisho wa kampuni hiyo kutoka nchini China inayojishughulisha na masuala ya bishara mtandaoni leo jijini Dar es Salaam. katika ni Mwenyekiti wa Chama cha Malkia wa Nguvu Tanzania,Grace Mpanduka
Afisa Tarafa wa Wilaya ya Ilala, George Anthony (kulia) akimkadhi zawadi mmoja wa washindi walio jishindia zawadi mbalimbali katika hafla ya utambulisho wa kampuni Longrich kutoka nchini China inayojishughulisha na masuala ya bishara mtandaoni leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Malkia wa Nguvu Tanzania, Grace Mpanduka wa (kwanza kuli) amewaomba wanawake kutunza ngozi zao kwa kutumia bidhaa za kampuni hiyo ambazo zinatengengenezwa kwa Mimea asilia kwa ubora wa hali ya juu.
washindi walio jishindia zawadi mbalimbal wakisoma vipeperushi mbalimbali leo katika afla ya utambulisho wa kampuni Longrich kutoka nchini China inayojishughulisha na masuala ya bishara mtandaoni leo jijini Dar es Salaam.
mkutano ukiendelea
Baadhi ya wangeni waliofika katika hafla ya utambulisho wa kampuni Longrich wakinunua bidhaa mbalimbali zinazo tengenezwa na kampuni hiyo.
picha ya pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...