Na Ripota Wetu,Michuzi Blog

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji amesema umefika wakati kwa Watanzania kuchukulia bima kama hitaji muhimu na kujifunza aina mbalimbali za bidhaa za bima zilizopo sokoni ili wazitumie kujikinga.

Dk.Kijaji amesema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya madarasa mawili, ofisi ya walimu na madawati 40 vyenye thamani ya jumla ya Sh.milioni 49 kwa Shule ya Msingi Lusangi iliyopo wilayani Kondoa,yaliyojengwa kwa msaada wa kampuni ya bima ya Sanlum, ambayo ndiyo mtoaji mkubwa wa bima barani Afrika.

“ Huduma ya bima inahitajika sana ili kuwawezesha watu kujikinga na majanga yasiyotabirika ya siku za usoni,” amesema Dk. Kijaji, na kuongeza ishara iliyoonyeshwa na kampuni ya Sanlam ya kurudisha sehemu ya faida yake kusaidia miradi ya jamii ichukuliwe kama ishara ya namna gani bima ni muhimu kwa uhakika wa maisha.

Amesema ni vema Watanzania wakapata elimu ya kutoa kuhusu masuala ya bima na faida zake ambazo kimsingi ni nyingi na zinamanufaa makubwa,hivyo ni wakati muafaka kwa jamii kutambua na kuona umuhimu wa uwepo wa bima.

Hata hivyo akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda – Afrika Mashariki wa Sanlam Pan-Afrika, Julius Magabe, amesema kampuni hiyo itaendelea kusaidia miradi ya jamii nchini Tanzania.

“ Naomba nichukue fursa hii kuwahakikishia kuwa Sanlam tutaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kutoa fedha kwa miradi mbalimbali ya jamii,"amesema Magabe, na kufafanua kampuni hiyo mwaka jana wa 2018 imesherehekea kutimiza miaka 100 tangu kuanziswha kwake na kwamba iko thabiti katika kurejesha sehemu ya faida yake kusaidia jamii.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lusangi, Josephine Paul amesema shule hiyo ilikuwa inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madarasa, kwa kuwa madarasa matano yaliyokuwepo kabla hayakuweza kutosheleza idadi ya wanafunzi ambayo ni 348.

“Kutokana na mradi huu kukamilika, utakuwa umepunguza changamoto ya upungufu wa madarasa na oofoso ya walimu uliokuwepo,” amesema Mwalim mkuu huyo.

Wakati huo huo uongozi wa Sanlam umesema wamefurahishwa na namna ambavyo fedha walizotoa kufanikisha ujenzi huo zimetumika kwa uadilifu mkubwa na kwamba wamethibutisha walivyowaamifu kwani Sh.milioni 2.7 hazijatumika kutokana na kupungua kwa gharama za vifaa vya ujenzi.Hata hivyo fedha hizo sasa zimeelekezwa zitumike kujenga vyoo vya wanafunzi wa kike na wakiume.

“ Sisi Sanlam hatujawahi kushuhudia mradi tunaoufadhili ukisimamiwa kwa umakini wa hali ya juu kiasi hiki,” amesema Magabe, ambayo kampuni anayotumikia ina matawi ndani ya nchi 38 barani Africa, huku huduma zake zikiwa zimesambaa mabara ya Amerika, Asia na Australia.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (kushoto) akipeana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima Sanlam kanda ya Afrika Mashariki, Julius Magabe wakati wa hafla ya makabidhiano ya madarasa mawili na ofisi ya walimu ya Shule ya Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bima Sanlam kwa thamani ya shilingi Milioni 49. Uzinduzi huo ulifanyika shuleni hapo tarafa ya Pahi, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma. Katikati ni Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), DK. Mussa Juma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima Sanlam Kanda ya Afrika Mashariki, Julius Magabe wakifungua pazia la jiwe la msingi kuzindua madarasa mawili na ofisi ya walimu ya Shule ya Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bima ya Sanlam yenye thamani ya shilingi milioni 49. Uzinduzi huo ulifanyika shuleni hapo iliyopo tarafa ya Pahi, Wilaya ya Kondoa, nkoani Dodoma. Kutoka Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life, Khamis Suleiman , Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Dk. Mussa Juma na Meneja wa Mamlaka hiyo Kanda ya Kati, Stella Rutaguza(kulia).
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bima Sanlam kanda ya Afrika Mashariki, Julius Magabe wakishikana mikono baada ya kufungua pazia la jiwe la msingi katika uzinduzi wa madarasa mawili na ofisi ya walimu ya Shule ya Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bima ya Sanlam kwa thamani ya shilingi Milioni 49. Uzinduzi huo ulifanyika shuleni hapo tarafa ya Pahi, Wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma leo. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life, Khamis Suleiman , Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Dk. Mussa Juma (wa pili kulia) na Meneja wa Mamlaka hiyo kanda ya kati, Stella Rutaguza (kulia).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...