Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha 

Shirika la Bima la Taifa(NIC) limekabidhi mabati 300 yenye thamani ya shilingi milioni nane laki moja kwa wilaya ya Arusha kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu mkoani Arusha. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha Mkurugenzi wa Shirika hilo Sam Kamanga alisema kuwa mabati hayo yanathamani ya shilingi milioni 8.1 na kuongeza msaada huo ni moja kati ya misingi ya utawala bora ambayo serikali inahimiza. 

Kamanga ameeleza kuwa ni mara ya kwanza kutoa msaada kwa Mkoa wa Arusha na kusema kuongeza kuwa tayari wameshatoa msaada katika mikoa mbalimbali ikiwemo Morogoro na Mwanza. 

Kamanga ameongeza kuwa wanatarajia kuja na bima ya kilimo watakayoizindua katika maonesho ya Nanenane mwaka huu mkoani Simiyu ambayo amesema ina lengo la kumkomboa mkulima. 

"tumeamua kuileta bima ya kilimo kwasababu wakulima wengi wamekua wanaingia katika kilimo na wakilima na kupata hasara wengine wanakata tamaa wengine wanakufa kwasababu ya presha ya kupata hasara hivyo ndio maana tumeleta msaada huu"alisema Kamanga

Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqaro alilishukuru shirika hilo kwa msaada kwakuwa utasaidia katika maandalizi ya uhitaji wa sekta ya elimu na kuziomba wizara nyingine kuitikia maombi waliyoomba. 

Alisema kuwa tangu serikali ya awamu ya nne itangaze elimu bure kumekuwepo na muamko wa wanafunzi na wazazi kupeleka watoto shule hivyo itawasaidia katika kuwekeza madarasa ya vyoo na nyumba za walimu 
Mkurugenzi wa Shirika hilo Sam Kamanga watatu kulia akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqaro mabati 300.
mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqaro akimkabidhi mkurugenzi wa jiji la Arusha dr Maulid Madeni mabati yaliotolewa na shirika la bima ya Taifa (NIC) mara baada yakukabidhiwa na shirika hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...