Moureen Rogath, Kibondo. 

Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, amesema hajafurahishwa na kasi ya mkandarasi wa kampuni ya Urban and Engineering Service aliyepewa tenda ya kusambaza umeme vijijini katika wilaya ya Kibondo na Kakonko mkoani Kigoma. 

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyange, kata ya Mabamba na kusema kuwa endapo mkandarasi huyo hatobadilika katika utendaji wake serikali itamchukulia hatua za kisheria.

Naibu Waziri alisema wilaya ya Kibondo ni vijiji 3 vilivyowashwa umeme kati ya 40 huku wilaya ya Kakonko vijiji 5 vimewashawa kati ya 29 na kwamba hadi June 2020 vijiji vyote vinatakiwa kuwaka umeme. 

"Dhamira ya serikali ni kuona watanzania wote wanapata umeme kwenye makazi yao na kuwataka wananchi katika maeneo ya vijijini kuchangamkia fursa hiyo," amesema Naibu waziri huyo. 

Mapema akizungumza mkuu wa wilaya ya Kibondo Louis Bura, ameishukuru serikali kwa kuipa kipaumbele wilaya hiyo kupata nishati umeme kwa mara ya kwanza katika kijiji hicho.

Hata hivyo mkanadarasi wa kampuni hiyo, Shuda Ndanya amesema kuwa kasi ya kazi ilipungua kwa muda kutokana na uhaba fedha kwenye kampuni uliosababisha baadhi ya vifaa kukwama bandarini jambo ambalo amedai kuwa tayari limepatiwa ufumbuzi na kuahidi kukamilisha kazi kwa wakati.

Mkazi wa kijiji hicho Rajabu Husein amesema kuwepo kwa umeme katika eneo lao utawasaidia wao katika kukuza shuguli za kuinua uchumi.
Naibu waziri wa nishati Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyange,  kata ya mabamba wilayani kibondo mkoani Kigoma
Naibu waziri wa nishati Subira Mgalu akizindua umeme kwa mara ya kwanza katika zahanati na kijiji cha Nyange , kata ya mabamba wilayani Kibondo mkoani Kigoma.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...