Katibu Mkuu mstaafu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Mussa Uledi akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 9, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo yaliyofunguliwa Julai 8, 2019 na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza. 
Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 9, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo yaliyofunguliwa Julai 8, 2019 na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza. 
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari- MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 9, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo yaliyofunguliwa Julai 8, 2019 na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza. 

Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 9, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo Bi Nelly Mtema akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo yaliyofunguliwa Julai 8, 2019 na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza..(Picha zote na Abubakari Kafumba, MAELEZO- Morogoro) 
………………… 

Na Frank Mvungi- MAELEZO- Morogoro 
Katibu Mkuu Mstaafu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Mussa Uledi amesema kuwa Tanzania inanufaika kiuchumi kama mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na jumuiya nyingine ambazo Tanzania ni mwanachama. 

Akizungumza wakati akiwasilisha mada leo mjini Morogoro ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo kwa waandishi wa habari ya kuwajengea uwezo wa kuandika na kuripoti habari za SADC, Bw. Uledi amesema kuwa nchi yetu imenufaika na utekelezaji wa miradi ya miundomnbinu, biashara, uwekezaji na viwanda. 

“ Mkakati wa maendeleo wa SADC unafafanana kwa kiwango kikubwa na ule wa Tanzania ambao pia unazingatia haja ya utekelezaji wa viwanda na miundombinu hapa nchini hali itakayochangia katika kuimarisha maendeleo na kukuza uchuni na ustawi wa wananchi” Alisisitiza Bw. Uledi 
Akifafanua amesema kuwa vipaumbele vya Tanzania vimejikita katika upanuzi wa Mauzo nje na uongezaji wa michepuo yake lengo likiwa ni kukuza na kuendeleza biashara hali inayowezesha uendelezaji wa viwanda vya kuongeza thamani katika malighafi za ndani hususan mazao ya kilimo na madini. 

Aliongeza kuwa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli katika baadhi ya nchi wanachama wa SADC imeonesha kuwa Tanzania imejipanga vizuri kimkakati inaweza kuwa ghala la Chakula kwa kukuza zaidi uzalishaji kuendana na mahitaji katika soko la jumuiya hiyo na hata nje ya jumuiya. 

Alitaja vipaumbele vingine kuwa ni pamoja na uendelezaji miundombinu kama barabara, reli, usafiri wa anga, uzalishaji na usambazaji huduma za umeme ambayo ni nyenzo muhimu sana katika kuyaunganisha masoko ya nchi wanachama wa SADC. 

Aliongeza kuwa vipaumbele vingine ni utafutaji wa rasilimali na utekelezaji wa miradi ya Kikanda kwa kuundwa kwa kikosi kazi cha Mawaziri wenye dhamana ya Fedha na uendelezaji miundombinu, Amani na Usalama umeendelea kuimarika ndani ya SADC. 

Tanzania inatarajiwa kuleta msukumo mpya kwa nchi wanachama wa SADC katika utekelezaji wa miradi na program za maendeleo za Jumuiya hiyo kwa kuwa itakuwa na dhamana kubwa ya kukidhi matarajio makubwa ya nchi wanachama wakati wote wa uenyekiti wake. 

Kwa upande wake Mkuu wa Operesheni na Mafunzo, Brigedi ya Magharibi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanali Wilbert Ibuge akiwasilisha mada katika mafunzo hayo amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi za mwanzo kabisa Barani Afrika zilizotoa mchango mkubwa na kuratibu kuanzishwa kwa mtangamano wa SADC. 

“Hadi sasa hali ya amani na usalama imeendelea kuimarika katika SADC kama inavyojidhihirisha kwa takribani nchi zote za SADC ambapo nchi wanachama ziliazimia kusimamia maendeleo ya kiuchumi ya Kanda kwa kuzingatia malengo ikiwemo kukuza uchumi, kuondoa umasikini, kuboresha hali ya maisha ya wananchi. 

Msingi wa SADC ni kusimamia malengo yake ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii sambamba na yale ya ulinzi na usalama unabainishwa katika Ibara ya 2 ya mkataba wa SADC ( Article 2 of SADC Treaty).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...