NA MWAMVUA MWINYI,PWANI


WATU wawili wamefariki dunia mkoani Pwani ,kutokana na matukio tofauti ya mauaji yaliyotokea wilaya ya kipolisi Chalinze, ikiwa ni pamoja na Damian Kimiti (70) ambae ameuawa kwa kupigwa shoka.

Kufuatia mauaji hayo watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapo. 

Akielezea kuhusiana na matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani hapo, kamanda wa polisi wa mkoa wa Pwani ,Wankyo Nyigesa alisema Kimiti aliuawa huko Malivundo ,Talawanda ,Chalinze, ambapo mtiliwa shaka Said Ngosha amekubali kuuwa na tayari amekamatwa .

Alisema ,baada ya mauaji muaji alipora simu tatu aina ya tecno ,solar panel moja,shuka na baiskeli."Pia alikubali kuonyesha simu tecno mbili ,solar panel moja na shoka moja"alifafanua Wankyo.

Katika tukio jingine ,Wankyo alieleza Ngurai Waziri (33) mfugaji huko Msolwa kijiji cha Lukenge aliuawa kwa kukatwa na visu.

Kamanda huyo alibainisha, mtiliwa shaka David Mwanje (28) , Thomas Gau (25) na Magoma Ramadhani Mbwiga (32) wamekamatwa na katika mahojiano ya awali watuhumiwa hao wamedai marehemu alikuwa mwizi wa mifugo na alikuwa kero katika wizi wa mifugo.

Wakati huo huo Wankyo alisema, juni 30 eneo la Sweat Corner Vigwaza katika barabara kuu ya Morogoro -Dar es salaam ,gari lenye namba za usajili T.182 DGH/T .182 DGM aina ya scania ,lililokuwa likitokea Iringa kuelekea Dar es salaam likiendeshwa na dereva Samwel Emanuel mkazi wa Makambako Iringa.

"Gari hilo liligongana uso kwa uso na gari lenye namba za usajili T.420 CGK/T.909 BZU scania lililokuwa likitokea Dar es salaam kuelekea Chalinze likiendeshwa na Iddi Rashid mkazi wa Tegeta ikiwa imebeba malighafi zitumikazo kutengeneza juice na kusababisha moto mkubwa na magari yote yaliteketea."aliongeza Wankyo.

Wankyo alitaja chanzo cha ajali ni gari lenye namba T.420 CGK aina ya scania kuhama upande wake na kuhamia upande wa kulia mwa barabara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...