Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

ASKOFU Mulilege Kameka Wa kanisa la Boko Yerusalem, kupitia kwa wakili wake John Mallya anatarajia kufungua upya kesi, Mahakamani dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji kufuatia Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kufuta maombi yake ya kutaka watu hao waletwe mahakamani hapo na kujieleza kwanini wasifungwe kwa kupuuza amri ya mahakama. 

Akizungumza nje ya mahakama baada ya uamuzi huo kutolewa, Wakili Mallya, amesema, ingawa maombi yao yamefutwa lakini bado hawajakata tamaa, atakwenda kuzungumza na mteja wake pamoja na mawakili wenzake ili kuona njia watakayotumia kufungua upya shauri hilo mahakamani.

Amsema bado wanaamini kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji wanakosa la kutotekeleza na kutii amri ya Mahakama ya kumuachia huru Askofu hiyo, 

"Jumanne tutakuja mahakamni kufaili kesi kama tulivyoelekezwa na jaji jinsi ya kufanya na kama kuna mtu yeyote anamaswali juu ya uraia wa mtumishi huyu wa Mungu aje mahakamani, " amesema Wakili Mallya. 

Kameka ambaye ni Askofu wa kanisa la House of Prayer Shield of Faith Christian Fellowship Church (HPSFCFC) maarufu kama Boko Yerusalem, anashikiliwa mahabusu kwa zaidi ya miezi tisa sasa kwa tuhuma za kutokuwa raia wa Tanzania, licha ya Mahakama Kuu kuamuru kuwa anapaswa kuachiwa huru kwani uraia wake hauna mashaka. 

Mapema leo Agosti 9,2019 Jaji Dk Atuganile Ngwala alitoa uamuzi wa kufuta maombi hayo kwakuwa yameletwa chini ya vifungu vya sheria ambavyo havihusiki.Akitoa uamuzi huo, Jaji Ngwala alisema, anakubaliana na hoja za mawakili wa serikali kuwa maombi hayo yalipaswa kuletwa chini ya kifungu cha 9 cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) badala ya kufungu namba 392 cha CPA na 114 cha sheria ya Kanuni ya adhabu.

Alisema kutokana na hali hiyo anayafuta maombi hayo kwakuwa hayajaletwa kisheria.Katika shauri hilo, Machi 18 Mwaka huu, Mahakama hiyo iliamuru askofu huyo aliyekuwa akishikiliwa na Wizara ya Mambo Ndani aachiliwe huru kutoka kizuizini anaposhikiliwa ikisema kwamba uraia wake hauna mashaka

Amri hiyo ilitolewa na Jaji IIvin Mgeta ambaye alitoa maelekezo kuwa Askofu hiyo atolewe mahali anaposhikili kwani vilelezo vilivyotolewa vimedhibitisha uraia wake kuwa ni mtanzania lakini licha ya amri hiyo kutolewa mpaka leo bado Askofu huyo ameshikiliwa na yuko mahabusu gerezani ndipo kupitia kwa Wakili wake Mallya aliamua kuyaleta maombi hayo.

Maombi hayo yamefunguliwa dhidi ya wajibu maombi ambao ni AG na Kamishna Mkuu Uhamiaji ambayo kabla ya kusikilizwa, upande wa serikali ukiongozwa na wakili wa serikali Jackline Nyantori waliwasilisha pingamizi la awali mahakamani hapo wakidai kuwa, Kifungu cha sheria ambacho wapeleka maombi wamekitumia kupeleka maombi hayo hakiipi mamlaka Mahakama Kuu ya kuweza kusikiliza maombi hayo .

Akijibu hoja hiyo, wakili wa mpeleka maombi, Mallya alidai kuwa maombi hayo yalipelekwa kwa mujibi na taratibu, kwani sheria inaruhusu kuleta maombi ya aina hiyo kwa njia ya hati ya maombi na kiapo kama walivyofanya wao katika kupeleka maombi.

Hata hivyo upande wa serikali ulisisitiza kwamba kwa kuwa kosa linalodaiwa kutendeka halikufanyika mbele ya mahakama waombaji walipaswa wapeleke malalamiko hayo kwanza polisi walete madai ndipo mahakama iyasikilize na kuyatolea maamuzi.

IAskofu Kameka anadaiwa kukamatwa na Wizara ya Mambo ya Ndani tangu Desemba,2018, kwa madai kuwa sio raia waTanzania, lakini alikuja hapa Mahakama Kuu Machi,2019 na mahakama hiyo ikaamua kuwa Askofu Kameka ni raia na uraia wake hauna mashaka hivyo Magereza na kitengo cha Uhamiaji wamuachie haraka amri ambayo mpaka leo haijatekelezwa. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...