MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama
Mwanamwema Shein amesema suala la matunzo ya wazee na ulezi wa
watoto linaendeana na utekelezaji wa Sera na Ilani ya Chama cha
Mapinduzi (CCM).

Amesema hayo katika hafla ya utoaji wa zawadi ya sikukuu ya Eid el
Hajj kwa wazee na watoto wanaoishi katika nyumba za Wazee Welezo
na Sebleni pamoja na vituo vya kutunzia watoto vya SOS na Mazizini,
alizozianda kwa kushirikiana na na Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Asha Suleiman Idd.

Akizungumza kwa niaba ya Mama Mwanamwema, Waziri wa Wizara ya
Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake wa watoto Moudline Castico
alisema katika kufanikisha malengo hayo Serikali inatumia zaidi ya
shilingi Milioni 200 kwa mwezi, ikiwa ni malipo ya Pensheni jamii kwa
wazee wenye umri wa miaka 70 na kuendelea.

Sambamba na hilo, alisema Serikali inaendelea kuyafanyia matengenezo
majengo ya makaazi ya wazee wasiojiweza ili kuleta ustawi bora wa
maisha yao, pamoja na kuwapatia huduma bure za afya ikiwa ni
kuthamini mchango mkubwa walioutowa wakati wa ujana wao.

Aidha alisema Serikali inakusudia kuifanya sheria dhana ya Pensheni
jamii, ili kuepuka athari za mabadiliko ya uongozi hapo baadae.
Alisema viongozi hao wameamuwa kutowa zawadi hizo ili kuhakikisha
wazee na watoto hao wanafurahi na kujumuika pamoja na wananchi
wengine.

Waziri Castico, aliwataka wazee hao kupitia sikukuu hiyo kuendelea
kuliombea dua Taifa, ili liweze kuepukana na athari zitokazo na majanga
mbali mbali.

Aidha, aliwataka wazazi na walezi kuzingatia malezi bora na maadili ya
ya watoto wao kwa kujiepusha na vitendo vya kikatili na udhalilishaji.

Alisema tukio la hivi karibuni la utupaji wa mtoto Kisiwani Pemba na
hatimae kuokotwa na mbwa, linathibitisha kwa kiasi gani jamii isivyojali
na kuthamini malezi na mtunzo ya watoto.

Alieleza kuwa Serikali imefanya juhudi kufanikisha upatikanaji wa
Mashine ya uchunguzi wa Vinasaba (DNA) ili kukabiliana na wimbi la
matukio mbali mbali ya udhalilishaji.

Mapema, Mkurugenzi wa kituo cha Kulelea watoto cha SOS, Asha Salim
aliwashukuru viongozi hao kwa muendelezo wao wa kila mwaka na
kuwatakia kheria na afya njema katika amisha yao.

Alisitiza umuhimu wa wazazi na walezi katika utunzaji wa watoto wao na
kuviomba vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na taasisi nyengine
zinazohusika na haki za watoto kuwachukulia hatua wote watakaobainika
kuhusika na vitendo vya udhalilishaji na utupaji watoto.

Nae, mtoto Salama Abdalla Ali wa kituo cha kulelea watoto Mazizini,
kwa niaba ya watoto wenzake aliwashukuru viongozi kwa imani na

mapenzi makubwa kwao na kuwakumbuka mara kwa mara, hatua
aliyosema inawapa faraja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...