Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja

Takribani vijana sitini (60) wanatarajiwa kuwasilisha Mawazo yao ya kibunifu katika shindano la kutekeleza malengo ya Maendeleo endelevu ya dunia hasahasa yakijikita lengo namba tatu, nne, tano, na nane. Malengo hayo yanazungumzia afya bora, elimu bora, usawa wa kijinsia na kazi za staha na ukuaji wa uchumi.

Bw.Naamala Samson akitoa mada kuhusu malengo ya Maendeleo endelevu

Shindano hilo lililopewa jina la THINNO CHALLENGE ikiwa ni muunganiko wa Think and Innovate yaani ‘Tafakari na Ubuni’, limezinduliwa rasmi tarehe 10 Agosti 2019 na shirika la Indelible Mark Movement. Tukio hili lilifanyikia kwenye ukumbi wa BUNI HUB iliyopo jengo la COSTECH, Kijitonyama jijini Dar Es Salaam.

Katika uzinduzi huo vijana kutoka vyuo mbalimbali zaidi ya kumi na sita (16) vya ndani na nje ya Tanzania na wajasiriamali mbalimbali waliweza kuhudhuria kupata mafunzo kuhusu malengo ya Maendeleo endelevu ya Dunia pamoja na kuhamasishwa kuwa na ari ya uthubutu na Ubunifu.

Bi.Alice Norberth kutoka Indelible Mark akiongea na washiriki

“Tunapotaka kuwa na kesho njema ni lazima kuhusisha vijana katika michakato yote hivyo ni lazima kuhakikisha wanaelewa vizuri matatizo kwenye jamii na kuja na Mawazo ya kibunifu kuyatatua Matatizo hayo, ndio maana tumeanzisha shindano hili, alisema Bi.Alice Norbeth, mwanzilishi wa shirika la Indelible Mark.

Kwa upande wake mkufunzi wa vijana hao, Bw.Naamala Samson ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Bella Africa, alisema,”Vijana ni zaidi ya asilimia sitini (60) ya idadi ya watu duniani hivyo ni muhimu kutumia vema nguvu kazi hii wajue nafasi yao katika utekelezwaji wa malengo ya Maendeleo endelevu ya dunia ili washiriki bila kuachwa nyuma”.

Mmoja wa washiriki hao, Bw.Issa Chapanga alionesha furaha yake na alisema yamemuwezesha kujitambua zaidi kwani palikuwa na mada kuhusu ‘kujitambua na uthubutu’. Mada hii iliwasilishwa na Dr.Nelsen Amar (PhD). Aliongezea kwamba pindi vijana wasikiapo fursa wasiziachie na wazichangamkie kwa haraka ili kujiletea Maendeleo wao binafsi na jamii kwa ujumla.

Shindano hili la THINNO CHALLENGE linatarajiwa kumalizika ifikapo mwishoni mwa mwezi wa tisa, ambapo washindi watapewa zawadi ikiwemo vyeti, tuzo na mafunzo mbalimbali kuwawezesha kutekeleza Mawazo yao.

Shirika la Indelible Mark Movement linaendesha shindano hili pamoja kwa ushirikiano na Taasisi mbalimbali kama Buni Innovation Hub, Bella Africa Consultancy, Raleigh Tanzania, Bridge For Change, ICS na linakaribisha wadau wengine kuunga mkono jitihada hizi kuongeza hamasa kwa vijana kuwa wabunifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...