Na, Editha Edward-Tabora 

Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Tabora mjini imefanya ukaguzi katika vyanzo vya maji katika Bwawa la Igombe linalotoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa manispaa ya tabora na kubaini uhalibifu katika baadhi ya maeneo ya vyanzo hivyo kutokana ba Shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwemo uvuvi na kilimo cha mbogamboga kinachodaiwa Kutumia viutatilifu ambavyo ni hatari kwa binadamu 

Mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Komanya Erick ameambatana na Wajumbe wa kamati hiyo ambapo wamekagua vyanzo hivyo vya maji na kupiga marufuku wakazi wa manispaa ya Tabora mjini wanaofanya Shughuli za kibinadamu ambazo wanafanya pembezoni mwa Bwawa hilo

Pamoja na hayo Komanya ametoa maagizo mbele ya kamati ya ulinzi kuwa wananchi wote ambao wamelima kando ya bwawa hilo wanatakiwa kufyeka mbogamboga pamoja na mazao mengine na kusafisha eneo hilo eneo liweze kuwa Wazi

"Natoa maagizo kwa mtendaji wa eneo hili ikifika kesho saa kumi na mbili jioni narudi kukagua hii Shughuli ya kilimo cha matango inayoendelea hapa na Shughuli zingine ni marufuku na ninaomba eneo hili ni la vyanzo vya maji tu Siyo Shughuli za kibinadamu tena na ninaomba viongozi muendelee kutoa elimu kwa Kushirikiana na TUWASA kuwa hili Siyo eneo la Shughuli za kibinadamu kwani mnasababishia watu wanapata maradhi ya kibinadamu kutokana na kumwagilizia mazao yenu madawa ya kemikali na mvua zikinyesha madawa yote yanaishia kwenye bwawa marufuku "Amesema Komanya

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi mjini Tabora TUWASA Mhandisi Joel Rugemalila amesema athari zinazojitokeza kutokana na Shughuli hizo za kibinadamu kama za kuchoma moto na kumwagilia dawa katika mimea ambayo imelimwa pembezoni na bwawa hilo ambapo mvua zikinyesha madawa yote yanatiririkia ndani ya bwawa hilo hivyo inaleta madhara makubwa kwa watumiaji

"Shughuli za kibinadamu pembezoni mwa bwawa hili zinasababisha madhara makubwa kwani ule udogo unakuwa tifutifu ambapo wanachoma kwa hiuo mvua zikinyesha uchafu wote unaishia kwenye bwawa na madhara yake yanapunguza kina cha bwawa ukishapunguza kina cha bwawa kinapunguza uwezo wa bwawa kutohudumia watu huduma ya maji kwa hiyo inakuwa ya shida sana" Amesema Rugemalila

Aidha bwawa la Igombe ndilo tegemeo kubwa kwa wakazi wa manispaa ya tabora na kwa sasa linakadiriwa kutoa huduma ya maji safi kwa wananchi wa manispaa hiyo zaidi ya laki tatu na nusu.
 pichani ni kamati ya ulinzi na usalama  iliyoambata na mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Komanya Erick katika ukaguzi wa bwawa la Igombe.
 Pichani ni Bwawa la Igombe  ambalo ndilo chanzo cha maji  linalotegemewa na wakazi wa Tabora mjini zaidi ya wakazi laki tatu na nusu.
 Pichani ni kilimo cha matango ambacho kimelimwa karibu na bwawa la Igombe ambapo mkuu wa wilaya ameagiza mimea hiyo ifyekwe.
Pichani ni kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Tabora mjini wakikagua eneo la bwawa la Igombe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...