Waziri Selemani Jafo,akizungumza kwenye ufunguzi wa Teachers day mkoa wa Dodoma iliyoandaliwa na benki ya NMB
Baadhi ya walimu Mkoa wa Dodoma wakishiriki Mkutano uliyoandaliwa na benki ya NMB

Waziri Selemani Jafo akikaribishwa na Meneja wa Kanda ya Kati NMB,Nsolo Mlozi.
Waziri Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja



………………….

Serikali imeitaja benki ya NMB kuwa miongoni mwa taasisi zilizofanikisha makusanyo ya fedha kwa mwaka 2018/19 kwa kuwa benki hiyo haina tofauti na Wizara ya Tamisemi kwa kufika maeneo yote nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) Seleman Jafo, wakati akizungumza na walimu zaidi ya 300 kutoka halmashauri za wilaya mkoani Dodoma katika siku ya mwalimu ambao walikutanishwa na benki ya NMB.

Waziri Jafo alisema uamuzi wa benki hiyo kwenda nchi nzima na kufungua matawi, mawakala pamoja na kuongeza ATM, ulisaidia kwa watu kuzifikia kwa urahisi huduma za kibenki pamoja na halmashauri kuitumia kwa makusanyo yake.

Hivi karibuni Jafo alitangaza mapato ya serikali kutoka katika halmashauri yakipanda kutoka asilimia 73 ya mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 81 mwaka 2018, juzi kwenye za mapato katika mmalaka ya serikali za mitaa tumekusanya takriban billioni 664 sawa na asilimia 91 kiasi ambacho hakijawahi kufikiwa. Ninyi NMB mmetusaidia kwa hili,” alisema Waziri Jafo.

Kuhusu benki ya NMB alisema ni miongoni mwa taasisi zinazofanya vizuri hapa nchini ikiwa na wateja zaidi ya 3.5 milioni pamoja na matawi 229 ambayo ni zaidi ya halmashauri zilizopo ingawa aliwataka waongeze wateja na kuagiza kitengo cha utafiti kufanya kazi yake vizuri.

Kuhusu mikopo alisema kuna kilio kutoka kwa watumishi kuhusu riba kubwa ya mikopo kwenye mabenki yote nchini kwani wanatoza kiwango ambacho si rafiki kwa wafanyakazi jambo linalopekea malalamiko na wengine kujutia uamuzi wa kukopa.

“Naomba suala la riba mliangalie, haiwezekani riba ya mfanyakazi ikawa sawa na anayefanya biashara, ndiyo maana mnasababisha walimu kuingia madeni kwenye visaccos vingine hadi wanaacha kadi zao huko mwisho wa siku wengine wanataka kujinyonga, tafakarini ikibidi mfike hata kwenye single digit,” alisema Jafo.

Katika hatua nyingine aliwataka walimu kutumia mishahara yao kwa utaratibu na kuacha maisha ya kuiga kwani ndiyo yanayowapelekea kwenye madeni makubwa.

Meneja wa NMB Kanda ya kati Solo Mlozi alisema benki hiyo imejipanga kuwafikia Watanzania mahali walipo kwa kutumia mawakala wake na kuendelea kuboresha huduma zao kwa kadri iwezekanavyo.

Mlozi alimwomba Waziri kufikisha ujumbe wao serikalini ili waendelee kuiamini benki hiyo na kufanya nayo kazi kwa kuwa serikali ina hisa ya asilimia 31 ndani yake hivyo na mambo yaliyozungumzwa watashauriana ili kuwapunguzia mzigo Watanzania.

Awali Meneja Mwandamizi wa wateja wadogo Ally Ngingite alisema benki hiyo imeweka utaratibu kuwafikia walimu kama sehemu ya wateja na kusikiliza changamoto zao.

Ngingite alisema mpango huo ulianzia Jijini Dar es Salaam,Pwani na jana Dodoma kabla ya kwenda mikoa mingine ikiwemo Zanzibar huku akitaja benki kusogeza huduma zaidi kw akutumia simu za mkononi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...