Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amesema Burundi haijakataliwa kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) ila bado haijakidhi vigezo.

Ameyasema hayo leo Agosti 21, 2019 jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na wahariri na waandishi wa habari nchini ambao alikutana nao kwa ajili ya kuwashukuru kwa kazi nzuri ambayo wameifanya kwa kuandika vema habari za mkutano Mkuu wa 39 wa SADC.

Pamoja na kutoa shukrani kwa waandishi wa habari nchini Tanzania kwa kazi hiyo nzuri, ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa ni vema akaliweka wazi suala la Burundi kuhusu kujiunga na SADC.

Amefafanua kuwa, wakuu wa nchi za jumuiya hiyo wamepokea ombi la Burundi la kutaka kujiunga na jumuiya hiyo lakini nchi hiyo imekidhi vigezo vya kujiunga kwa asilimia 70 na imebaki asilimia 30 ambayo watatakiwa kukamilisha.

"Waandishi wa habari ifahamike nchi ya Burundi haijakataliwa ila bado hawajakidhi viwango, ukiwa mwanachama kuna ada na katika kigezo hicho bado hawajakidhi, hivyo watajiunga baada ya kukidhi vigezo vilivyopo ndani ya jumuiya hiyo,"amesema Waziri Kabudi.

Wakati huo huo Waziri Kabudi amewashukuru waandishi wa habari, wahariri na vyombo vyote vya habari nchini kwa namna ambavyo wameungana kufanikisha jambo hilo kubwa la kitaifa.

"Tunawashukuru waandishi na wahariri wote wa habari nchini, mmefanya jambo kubwa kwa ajili ya nchi yetu. Mmehakikisha mkutano wa SADC unafanikiwa na kweli mmeonesha uzalendo mkubwa kwa nchi yetu.Tumeungana sote kwa umoja wetu na hapa nishauri kwenye mambo yanayohusu Taifa tuwe wamoja,"amesema Waziri Kabudi.

Amesisitiza waandishi wa habari wamehakikisha Afrika na Dunia inafahamu kila kinachoendelea kwenye mikutano ya SADC na kueleza kuwa sasa kazi ndio imeanza kwani Tanzania kuwa Mwenyekiti wa jumuiya hiyo kuna vikao 32 ambavyo vitafanyika nchini. 

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi akifafanua mbele ya Wakuu na Wahariri Wakuu wa Vyombo vya habari, leo katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar,kuhusu  nchi ya Burundi  kukataliwa kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC),ambapo ameeleza kuwa nchi hiyo haijakataliwa, ila bado haijakidhi vigezo.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi leo Agosti 21, 2019 jijini Dar es Salaam akizungumza na wahariri na waandishi wa habari nchini ambao alikutana nao kwa ajili ya kuwashukuru kwa kazi nzuri ambayo wameifanya kwa kuandika vema habari za mkutano Mkuu wa 39 wa SADC.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi  akipewa mkono wa Pongezi  kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Damas Ndumbaro  mara baada ya kuzungumza na  Wakuu, na Wahariri Wakuu wa Vyombo vya habari, leo katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar.Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...