Na Editha Edward-Tabora 

Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani ameuagiza uongozi wa shirika la umeme Tanesco mkoa wa Tabora kuanza kuwalipa fidia wananchi wa vijiji vinne vya kata ya mwisi vilivyopo wilayani Igunga mkoani Tabora waliopitiwa na mradi wa umeme wa REA ambapo ameweka bayana kuwa zaidi ya Shilingi bilioni miatatu tayari zimetengwa kwa ajili ya kuwalipa wananchi hao 

Dkt, Kalemani akiwa katika kijiji cha mwisi Wilayani Igunga mkoani Tabora amefanya mkutano wa hadhara katika kijiji hicho ambapo mmoja wa wananchi anaeishi katika kijiji hicho, Hamis Masinge amepewa fursa kueleza malalamiko yao ya kudai fidia kwa muda mrefu "Tumesumbuka sana sisi wananchi wa kata hii tumekutafuta sana waziri wa umeme lakini Bila mafanikio tumeshindwa kukarabati majumba yetu mabovu yako barabarani na wakati wote yanaweza kuvunjika kwa hiyo tunogopa kukarabati na tusipokarabati tunaweza kupondwa na hayo majumba waziri tunaomba utusaidie"Amesema Masinge

Kwa upande wake Meneja wa Tanesco Tabora Mhandisi Alvin Limo amesema Sababu ambayo ilikuwa inawakwamisha wananchi kutopewa fidia hizo ni uhakiki ambao walikuwa wanafanya shirika hilo"Tulikuwa tunafanya uhakiki kwa wananchi kwani Mwanzoni kulikuwa kuna watu ambao walijiingiza katika orodha hiyo ndo maana tulichelewa kuwalipa fidia zao kw waliopitiwa na mradi huo"Amesema Limo

Aidha pamoja na hayo Waziri Kalemani amezindua na kuwasha umeme wa REA katika kijiji cha Isenegeja wilaya ya Igunga huku akitoa wito kwa wananchi Kutumia nishati hiyo kwa Shughuli za maendeleo na Kutunza pia miundo mbinu Ili kuleta mabadiliko katika Sekta ya uchumi.
 Pichani ni waziri Wa nishati dkt. Medard Kalemani akiwasha umeme wa REA katika kijiji cha Isenegeja wilayani Igunga.
Pichani ni moja kati ya nyumba iliyopata umeme Wa REA   katika kijiji cha Isenegeja wilayani Igunga.
 Pichani ni waziri wa nishati Medard Kalemani Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwisi wilayani Igunga mkoani Tabora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...