Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mkazi wa Buguruni, Thomas Mgoli (37) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  akikabiliwana na kesi ya Uhujumu Uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la kujifanya Afisa Usalama wa Taifa anayetaka kumsaidia aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Kelvin Mhina na wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi akisaidiana na wakili wa serikali mwandamizi Wankyo Simon, amedai kuwa, katika shtaka la  kwanza imedaiwa, katika tarehe tofauti kati ya Desemba 1, 2017 na Agosti 2019 katika eneo la Mahabusu ya Keko, huko Temeke, mshtakiwa alijifanya kama Mtumishi wa Umma aliyeajiriwa kitengo cha Usalama wa Taifa (TISS)

Katika shtaka la pili imedaiwa kuwa, kati ya Agusti 17 na 29,2019 katika maeneo tofauti ndani ya jiji la Dare es Salaam,  mshtakiwa kwa njia ya kudangaya alijipatia  Sh. 280,500 kutoka kwa Lucy Ngongoseki kupitia  namba mbili za simu tofauti za mtandao wa Airtel akijifanya kuwa yeye Afisa Usalama kutoka TISS  anayetaka kusaidia kesi namba 213/2017 ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Jamal Malinzi katika mahakama ya Kisutu kwa ajili

Aidha katika kosa la   mwisho imedaiwa, siku na mahali hapo, mshtakiwa alijipatia fedha kiasi cha sh 280,500 huku akijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi  la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu

Hata hivyo,  baada ya kusomewa mashitaka hayo, Hakimu Mhina alisema mahakama  hiyo haina mamlaka ya  kumpatia mshitakiwa dhamana, pia haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi hivyo mshtakiwa atakwenda rumande.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo basdo haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 4, 2019.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...