Benki ya Exim Tanzania leo imezindua kampeni maalum inayolenga kuhamasisha wateja wake kuhusiana na matumizi ya mtiririko wa huduma maalumu za kiusalama kwenye masuala ya fedha zinazotolewa na benki hiyo.

Kupitia mtoririko huo imebainishwa kuwa wateja wa benki hiyo wanapata huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya usafirishaji wa fedha kwa usalama (Cash-In-Transit service), huduma ya kiusalama ya malipo (Host to host services), huduma za kisasa za hundi (Corporate Cheque Capture service) pamoja na huduma ya kuweka (deposit) pesa kwenye akaunti ya benki hiyo wakati wowote kwa kutumia mashine ya kuwekea fedha (Cash Deposit Machines services). 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Mkuu wa Idara ta Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Bw Stanley Kafu alisema kupitia huduma hizo wateja wa benki hiyo hawahitaji tena kupanga foleni kwenye matawi ya benki hiyo ili kupata huduma za kifedha au hata kuhofia muda wa kufungwa kwa huduma za benki hiyo kwa kuwa wanaweza kupata huduma wakiwa kwenye maeneo ya kazi. 

“Huduma hizi ni sehemu ya mkakati wa benki ya Exim Tanzania kutoa huduma kwa wateja bila kubanwa na muda wa kazi au umbali wa kijiografia.,’’ alisema Kafu 

Akifafanua kuhusu huduma ya usafirishaji wa fedha kwa usalama (Cash-In-Transit service), Kafu alisema inamuondolea mteja hatari (risk) ya kuibiwa, kuvamiwa, kunyang’anywa pesa wakati anazitoa ofisini kwake kupeleka benki kwa kuwa atapatiwa huduma ya kusafirisha fedha hizo kuelekea na kutoka benki kwa kutumia usafiri maalumu ukiwa na walinzi wenye mafunzo maalum ya kulinda fedha. 

“ Kupitia huduma yetu ya Host- to- Host service, mteja wetu anaruhusiwa kutumia matawi yetu yote Tanzania nzima kupokea malipo yake ya invoices kutoka kwa wateja wake wote nchi nzima. Huduma hii ni kwa wateja ambao wanatoa na kupokea hundi nyingi kutoka kwa watu mbalimbali kama vile vyuo vikuu, mashule, viwanda, kampuni za usafirishaji, kumpuni za clearing and forwarding, biasahara za mitandaoni, shughuli kama hoteli na utalii.’’ alitaja 

Aidha akizungumzia huduma ya ‘corporate cheque capture’ Kafu alisema hudumahiyo inayotumia ‘scanner’ inamuwezesha mteja kuweka hundi zake (deposit cheque) wakati wowote bila kutembelea tawi lolote la benki. 

“Hakuna haja ya kupanga foleni tena, huduma ipo ofisini au nyumbani kwako. Huduma hii ni maalumu kwa wateja wote wenye biashara ambazo zinapokea hundi (cheque) kwa wingi kila siku bila kujali ni shilingi za kitanzania ama dola za kimarekani, au inatoka benki gani hapa Tanzania. Hapa tunahusisha biashara kama za usafirishaji, mashirika ya bima, wauza magari au pikipiki na vipuli, maduka ya jumla, mawakala wa gesi, pamoja na viwanda mbalimbali.’’ Alitaja. 

Kuhusu huduma ya mashine ya kuweka fedha (Cash Deposit Machine), Kafu alisema , inamsaidia mteja kuweka (deposit) pesa kwenye akaunti ya benki hiyo wakati wowote bila kutembelea tawi la benki ambapo mteja akishaweka pesa katika mashine hiyo anapata risiti ambayo inaonyesha kuwa pesa tayari imeshaingia kwenye akaunti, na kisha mteja anaweza kuendelea kufanya miamala kama vile kutoa (withdraw) au kutuma malipo mbalimbali. 

“ Mashine hii inafanya kazi masaa 24 siku saba za wiki hivyo hakuna haja ya kupanga foleni tena, huduma ipo ofisini au kiwandani kwako. Huduma hii inamuondolea mteja risk (hatari) na wasiwasi wa kuibiwa, kuvamiwa, kunyang’anywa pesa wakati anazitoa ofisini kwake kupeleka benki.’’ Alisema. 

Aliongeza kuwa benki hiyo itaendelea kubuni huduma za kisasa zaidi ambazo si tu zinaokoa muda kwa wateja hao bali pia kuwahikikia usalama wao na fedha zao ili kwenda sambamba na kauli mbui ya benki hiyo inatosema “ Exim Tupo Kazini Leo Kwa Ajili Ya Kesho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...