Kamanda wa Polisi wa Kikosi Cha Polisi cha Usalama Barabarani Gabriel Chiguma akizungumza na madereva katika Stendi Kuu ya mabasi Mjini Tabora mara baada ya kufanya ukaguzi wa mabasi.
 Askari wa Kikosi Cha Usalama barabarani akionesha abiria namna Mfumo wa gari kuwa kabla ya haijaanza safari.
Mkaguzi wa mabasi Hamis Mshihiri akizungumza na waandishi kuhusiana namna wanavyofanya ukaguzi katika mabasi kabla hayajaanza safari.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii Tabora
KIKOSI cha Polisi cha usalama Barabarani  Mkoani Tabora kimesema kuwa madereva wafuate sheria za usalama barabarani katika kuepusha ajali zinazotokana na uzembe wa kibindamu.

"Nitakula sahani moja na madereva wazembe ikiwa ni kulinda usalama wa abiria pindi wanaposafiri kwenda katika shughuli mbalimbali"amesema Chiguma.

Hayo ameyasema Kamanda wa polisi wa Kikosi hicho Gabriel Chiguma wakati akizungumza na madereva katika Stendi Kuu ya Mabasi Mjini Tabora, Chiguma amesema kuwa madereva waachane na ulevi wakati wa kuendesha vyombo vya moto.

Amesema kuwa agizo la kutembea usiku madereva wanalitumia vibaya kwa kuongeza mwendo.

Chiguma amesema hakuna sababu yeyote itakayofanya dereva asichuliwe hatua kutokana kutumia vibaya agizo la serikali la kutembea usiku.

Aidha amesema kuwa madereva ni wajibu wao kuendesha mabasi kwa weledi ili kulinda usalama wa abiria na mali zao.

Chiguma kuwa Tabora isiyokuwa na ajali inawezekana na hivyo atasimamia katika kuhakikisha madereva wanafuata sheria za usalama barabarani na wataokwenda kinyume watanyanganywa leseni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...