Charles James, Michuzi TV

KATIKA kuhakikisha Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma inapiga hatua kutoka kufanya kilimo cha kujitegemea na kufanya kilimo cha uchumi, Mkuu wa Wilaya hiyo amewataka wakulima kuunda ushirika wao.

DC Ndejembi amesema sehemu yoyote ambayo watu wamefanikiwa kimaendeleo ni kwa sababu waliamua kuungana na kushirikiana.

Hayo ameyasema katika uzinduzi wa uuzaji wa matrekta ya kilimo wilayani humo uliofanywa na Kampuni ya Loan Agro ambao ni wauzaji wa matrekta ya John Deere sambamba na Mabenki washirika ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) na Benki ya NMB.

" Niwaase wakulima wote wakubwa tuthubutu, tuanzishe ushirika wetu huu ndio utatusaidia kuwa na mawasiliano mazuri na wenzetu wa mamlaka ya hali ya hewa, watu wa mbegu bora na watafiti wa Ardhi hapa ndipo tutakapoona faida ya kilimo, bila ushirikiano huo ni ngumu kufanya kilimo cha uchumi.

Haya mabenki ambayo tunayalalamiki kuwa wana riba kuwa siku tukiwa na ushirika wetu wao ndio watakua wakitufuata na kutuomba tuchukue mikopo kwao kwa riba nafuu," Amesema DC Ndejembi.

Amesema ni wakati sasa pia kwa wakulima wa wilaya hiyo kuanza kulima zao la korosho ikiwa ni muendelezo wa kampeni yao kama wilaya ya kuondoka njaa 

" Korosho ni zao la thamani sana kwa sababu ni la kudumu hivyo uthaminishwaji wake una thamani sana katika kukopesheka na mabenki na unakua rahisi, " Amesema DC Ndejembi.

Kwa upande wake Afisa Biashara wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini, Willy Lyumi amesema Benki yao itaendelea kuwa pamoja na Wakulima katika kuhakikisha wanapiga hatua kutoka kufanya kilimo cha kujitegemea na kufanya kilimo chenye faida kiuchumi.

Amesema leo la Benki ya TADB ni kubadilisha aina ya kilimo cha mazoea ambacho kinafanywa na Wakulima wengi nchini lakini pia kuhakikisha Nchi inakua na chakula cha kutosha.

" Sisi tunatoa mikopo kwa wakulima mbalimbali lengo likiwa kukuza kilimo ambacho sisi kama TADB tunaamini ndio uti wa mgongo wa Taifa letu katika kukua kiuchumi.

" Tunafahamu dhamira ya Serikali yetu ya awamu ya tano chini ya Dk John Magufuli imejipanga kuifanya Nchi yetu kuwa Nchi yenye uchumi wa kati na Kilimo ni mojawapo ya sekta muhimu katika kufikia malengo hayo, na sisi kwa kutambua dhamira hiyo njema ya Mhe Rais ndio maana tunahakikisha wakulima wananufaika na Benki hii ambayo ni mahususi kwa ajili yao," Amesema Lyumi.

Aidha amewataka wakulima kutoogopa kukopa na kuwahakikishia kuwa wao kama Benki inayojali maslahi ya wakulima inatoa ushauri kwa mkulima yeyote anayeenda kuomba mkopo kabla ya kumpatia hiyo ni katika kumfanya mkulima afaidike na uwepo wa Banki ya Maendeleo ya Kilimo.

Nae Margret Julius ambaye ni Afisa Mauzo Mkuu wa Kampuni ya Loan Agro amemhakikishia DC Ndejembi kuwa watauza matrekta hayo kwa bei nafuu ambayo kila mkulima ataimudu lakini pia upatikanaji wa vifaa vyake utakua rahisi na wa bei nafuu.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa (katikati), Mhe Deo Ndejembi akikata utepe kuashiria kuzindua uuzaji wa matrekta ya kilimo wilayani Kongwa leo.

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe Deo Ndejembi akizungumza wakati wa uzinduzi wa uuzaji wa matrekta ya kilimo katika eneo la Kibaigwa wilayani humo leo
 Afisa Biashara kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Nchini (TADB), Willy Lyumi akizungumza katika uzinduzi huo ambapo ameahidi Benki hiyo kuendeleza ushirikiano na Wakulima katika kukuza sekta ya Kilimo
 Baadhi ya wakulima wa Wilaya ya Kongwa waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa matrekta ya kilimo wilayani Kongwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...