amanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Mulilo Mulilo 

Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MCHIMBAJI mdogo wa madini ya dhahabu aliyefahamika kwa jina la Ndaki Juma(45), amefariki dunia huku wengine nane wamejeruhiwa baada gema la machimbo ya madini ya dhahabu katika duara namba 50 yaliyopo Kata ya Inonelwa wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza kuangukiwa na kifusi wakati wakiendelea na shughuli za uchimbaji madini.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Mulilo Mulilo amewaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo limetokea Septemba 9,2019 saa moja asubuhi katika machimbo hayo ya dhahabu Shilalo, yaliyopo kata ya Inonelwa wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza wachimbaji wadowadogo wakiwa kwenye shughuli zao za kawaida za uchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu katika duara namba 50 mali ya Deogratius Ushanga na duara namba 47 g mali ya Peter Charles, duara zilizo kuwa na wachimbaji takribani 10.

Amewataja wachimbaji waliokuwa kwenye machimbo hayo ni Ndaki Juma (45) , Nyamikoma-busega, Keo Werema (34)John Katwale( 35), Mwita George (27), Masanja Charles ( 42) Abdallah Abdu(38), Bengwe Clenent(29), Songa Charles(28) Emmanuel Mathias(34) na Mang’era Meki(40).

"Wakati wakiendelea na uchimbaji ndani ya maduara hayo ghafla gema la udongo lilimeguka, likaporomoka na kuanguka kisha kufunga njia za maduara hayo. juhudi za haraka zilifanyika na kufanikiwa kuwaokoa watu wanane wakiwa hai,wakiwa na majeraha mbalimbali na mtu mmoja alikutwa amefariki ambae ni Ndaki Juma na jitihada za kumuokoa mtu aitwaye Keo Werema zinaendelea kufanyika. Majeruhi walifikishwa hospitali ya wilaya Misungwi kwa matibabu na maiti imehifadhiwa hospitalini kwa hatu za uchunguzi,"amesema Kamanda Mulilo.

Katika tukio lingine Kamanda Mulilo amesema tarehe 06/08/2019 ,saa saba maeneo ya Mtaa Kagera jirani na Shule ya msingi Kagera wilayani Ukerewe kulitokea tukio la mauaji ambapo Euzebia Didakus Malas (16) ambaye ni mwanafunzi kidato cha tatu shule ya sekondari Nansio aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani.

Amesema Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata Joseph Msafiri Anthon(30) mkazi wa mtaa wa Kagera Nansio ambaye ni Mwalimu wa shule ya msingi Namabugo, uchunguzi wa awali unaonesha kumtuhumu mwalimu huyo kuhusika na mauaji hayo.

Wakati tukio la tatu limetoa Septemba 7, mwaka 2019 huko wilayani Sengerema katika ufuatiliaji walikamatwa watuhumiwa wanne kuhusiana na tukio la kuvunja nyumba usiku na kuiba silaha aina ya rifle lililotokea Septemba 2 mwaka 2019 huko kijiji cha Isaka kata ya Nyehunge ambapo silaya yenye namba nyg/ir/95/2019 imekamatwa na watuhumiwa James Juma(20) , Alex Panda( 49), Shaban Mohamed (42) na mapambano Charles( 35).

"Baada ya kuwakamata watuhumiwa waliwapeleka askari katika eneo la Isaka Nyehunge na kupelekea kupatikana kwa silaha rifle yenye namba a 6986 ambayo ni kilelezo kilicho ibiwa katika tukio tajwa,"amesema Kamanda.

Pia Kamanda Mulilo amesema Agosti 15 mwaka huu wa 2019 katika eneo la Mahina mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Mahina Martha Joseph(16) alikutwa ameuawa baada ya kubakwa na kisha mwili wake kutelekezwa sehemu yenye mawe mengi. 

"Watuhumiwa wafuatao wamekamatwa na kukiri kuhusika na mauaji hayo ambapo ni Sospeter Kazumari (37), Jastine John ( 24), Amos Andrea(36) na Rebeka Bukindu (35,"amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...