Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imekataa ombi la upande wa utetezi la kuahirisha  kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema ikiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe na wenzake kwa siku 20.

Pia imesema katika kesi hiyo kumekuwa na migogoro kuanzia kusikilizwa hadi wakati wa kuahirisha.

Akiahirisha kesi hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema kuwa kesi hiyo haiwezi kuendelea kwa siku tatu zilizopangwa kuanzia jana, leo na kesho (Septemba 19,mwaka huu)  kutokana na sababu zilizotolewa na upande wa utetezi  kwamba mawakili wapo Mahakama Kuu na washitakiwa wawili wamefiwa.

Hakimu Simba amesema anaamini hati za wito zilizotolewa mahakamani hapo ni sahihi na kwa maelezo ya mshitakiwa Peter Msigwa amefiwa na bibi yake mkoani Iringa na John Heche amefiwa na mtoto wa kaka yake Musoma.

Amesema, analazimika kuahirisha kesi hii lakini kwa sababu zilizotolew na upande wa utetezi lakini haridhishwi kuahirisha kesi hiyo kwa siku 20 kwa sababu wakili hajapeleka udhibitisho kwamba mawakili watakuwa busy mpaka Oktoba 7 na 10, mwaka huu kama walivyoomba tuahirishe lakini pia katika kesi hiyo kuna jopo la mawakili wengi.

"Kesi hii imekuwa ikiahirishwa mara kwa mara na kusababisha mahakama kulalamikiwa kwa kuchelewesha kesi hivyo, ni lazima wahakikishe wanamaliza kesi kwa wakati", amesema Hakimu Simba.

Aidha ameongeza kuwa, migogoro inayotokea imesababisha kesi hiyo ichelewe mpaka sasa pamoja na kwamba ilianza kusikilizwa kwa hakimu mwengine

Kesi hiyo itaanza kusikilizwa utetezi kuanzia Septemba 24 hadi 27 na Oktoba Mosi na 10 mwaka huu.

Mapema, wakili wa utetezi, Gaston Garubindi alidai mawakili wa utetezi wanaosikiliza kesi hiyo, Peter Kibatala anakesi zingine ahakama Kuu mbele ya Msajili Tiganga na Profesa Abdallah Safari yupo Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga mbele ya Jaji Cyprian Mkeha na Hekima Mwasipu yupo Mahakama Kuu Tanga.

Pia amedai Msigwa na Heche wamefiwa na ndugu zao na wameomba kuondoka mchana wa leo (jana) hivyo, kesi hiyo haiwezi kuendelea na kuomba mahakama iahirishe kesi hiyo hadi Oktoba 7 au 10, mwaka huu.

Hata hivyo,  Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alidai washitakiwa hao wanawakilishwa na mawakili wengi ambao mahakama haijaelezwa wako wapi  endapo mahakama itapendekeza kuahirisha kesi hiyo, lipangwe kwa haraka kwa sababu muda walioomba upande wa utetezi ni mrefu.

Mbali ya Mbowe washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu Taifa, Dk Vincent Mashinji ,  Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu,  Mbunge wa Kibamba, John Mnyika,  Katibu Mkuu Taifa, Vicent Mashinji na Mbunge wa Kawe  Halima Mdee.

Wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.

Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, Februari Mosi na 16, mwaka jana, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...