MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mapema leo alipotembelea kituo cha Clouds FM kupitia kipindi cha XXL, alisema kuwa siku ya kwanza kupata taarifa kuwa amechaguliwa kuwa Mkuu wa Mkoa alikuwa anatoka Hospitali ya Mwananyamala kukagua wadi za watoto.

“Nakumbuka siku hiyo nilikuwa nimetoka Mwananyamala Hospital kuangalia wodi za kina-mama wajawazito ambao wapo Mwananyamala na sehemu za 'Operation Room' sio rafiki kwao, hivyo nilienda kuangalia namna gani tunaweza kuziboresha nikiungana na wadau wengine.

Baada ya hapo nikarudi nyumbani, lakini wakati nipo seating room na kijana mmoja aitwae  Rey wa hapa @cloudstv ndiyo akaniambia Mh naona hapa umechaguliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kiukweli sio kitu ambacho nilikuwa natarajia hivyo kilinishtua sana, kwani kutoka kuwa mkuu wa Wilaya mpaka mkuu wa mkoa halikuwa jambo ambalo linawezekana sana kwangu” 

Anaendelea kuelezea Mkuu wa mkoa wa Dar, Paul Makonda, namna ambavyo yeye anaweza kutofautisha kazi yake na maisha ya familia. 

“Mimi ni Baba mzuri kwa familia yangu pia ni mume mzuri na mke wangu anafahamu hilo, siwezi kupeleka stress za kazini nyumbani kuna baadhi ya mambo huwezi ku- share na mke wako kama hana hekima ya ki- Mungu, maana utayasikia kwenye saloon, hivyo kiapo ambacho niliapa mwenyewe hivyo mambo ya kazi yanabaki kazini na nikirudi nyumbani nakuwa baba na mme bora.” 

“Ila watu wanatakiwa kujua tu kuwa siku zote mimi nimekuwa nikieleza mambo yanayoendana na uwepo wa jamii yetu hivyo utaona kutoa kwangu kibari kwa wachungaji kwenda kuhubiri sehemu za kumbi za starehe nafahamu kabisa wazi kuwa katika maisha ya siku hizi kuna watu wengi huwa wanakwenda Club wakiwa na mawazo yao kule sasa wakikutana na neno la Mungu wanaweza kupona, ila sijamlazimisha Mtumishi yoyote kuhubiri kwenye Club," Alisema Paul Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mapema leo alipotembelea kituo cha Clouds FM kupitia kipindi cha XXL

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...