Na Mwandishi wetu, Globu ya Jamii
ALIYEKUWA Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi ameieleza mahakama ya hakimu mkazi  kisutu  kuwa alikuwa akilipwa fedha na TFF kwa taratibu za uendeshaji wa shirikisho hilo na wala hajawahi kujaza fomu ya madai ya ulipwaji wa fedha  na wala hajawahi kutoa maelekezo ya jinsi ya upokeaji wa fedha hizo.

Malinzi ameeleza hayo leo Septemba 18,2019 mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde  wakati akijibu maswali ya wakili  wa serikali kutoka Takukuru Leonard Swai.

Amedai kuwa fedha hizo zililipwa kupitia kwa Shadi wa 10 Hellen Ushahidi wa 12 Miriamu Zayumba na nyingine zilikuwa zikiingizwa kwenye akaunti.

Amedai katika shtaka la 16-25 inaonyesha kuwa alilipwa fedha na TFF, lakini  fedha hizo zililipwa kwa utaratibu na sio kweli kwamba aliwahi kutoa maelekezo ya upokeaji wa fedha hizo na kuongeza kudai kuwa, hundi na vocha zilizotolewa mahakamani ni baadhi kwani kuna zingine hazikuletwa mahakamani kama ushahidi.

Akiendelea kutoa ushahidi alidai aliwahi kufadhili mbio za wabunge (bunge marathon) kwa mika 7 toka miaka1997 hadi 2004 kuutangaza mchezo wa ngumi,mchezo wa golfu  pamoja na kujenga uwanja.

Amedai wakati anafadhili mbio hizo, Spika wa wakati huo pamoja na mwenyekiti wa bunge hawakumbuki ila anayemkumbuka ni  kiongozi wa timu hiyo  marehemu Joeli  Bendera na baadae alifuatiwa na William Ngeleja na kwamba fedha zilitoka Cargo Star na nyaraka za kumkabidhi fedha Bendera  na Ngeleja zipo Cargo Star.

"Fedha  hizo kwenye risiti zilikuwa zikiandikwa kulipwa mkopo na  nyingine marejesho ya mkopo na wala sikuwahi kumkabidhi mtu yoyote nyaraka za malipo" amedai 

Malinzi bado anaendelea kuhojiwa kutokana na ushahidi wake wa utetezi, kesi hiyo itaendelea kesho

Mbali na Malinzi, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa, Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga na Karani Flora Rauya.

Katika kesi  hiyo ya jinai namba 213 ya mwaka 2017 washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 20 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa Dola za Marekani 173,335.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...