Na Woinde Shizza,Arusha

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera, amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano kama timu, bila kujali nafasi walizonazo, ili kufikia malengo ya yaliyoaanishwa kwenye mpango mkakati wa halmashauri hiyo.

Ametoa rai hiyo alipokutana na watumishi wa sekta zote za halmshauri hiyo, katika kikao kazi cha kawaida, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo, mwanzoni mwa wiki hii.

Mkurugenzi Dk. Mahera amefafanua kuwa lengo la kikao hicho ni kukumbushana wajibu na majumumu ya kila mtumishi, kwa kujengeana uelewa wa pamoja kwa watumishi wote katika uwajibikaji wenye tija ya kufikia malengo ya Serikali ya kuwahudumia wananchi wa halmashauri hiyo pamoja na kujadili changamoto zinazokwamisha utendaji kazi.

Pia amewakumbusha watumishi hao, kutambua kuwa utumishi wa umma ni dhamana waliyopewa na Serikali, na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni, sheria, taratibu na za utumishi wa umma pamoja na miongozo ya serikali, kwa kutumia taaluma zao katika kutekeleza majukumu yao, kwa kuzingatia haki na usawa.

"Serikali imewaamini na kuwapa dhamana ya kuwatumikia wananchi, tumieni taaluma zenu kutekeleza majukumu yenu, tushirikiane kama timu ili kuijenga Arusha DC na Serikali yetu kwa ujumla" amesema Dk. Mahera.

Sambamba na hayo Dk. Mahera amewaagiza Maafisa watendaji wa kata, kusimamia suala la usafi wa mazingira na kuhakikisha wananchi, wanatozwa tozo stahiki za taka na kupewa risiti za fedha zilizolipiwa, sambamba na kuwachukulia hatua za kisheria, wananchi ambao wanakaidi na kunyanyasa wengine.

Kwa upande wa Mkuu wa Idara ya Utumishi katika halmashauri hiyo ya Arusha Hamis Mpume, amewaahidi watumishi hao kuendelea kusimamia haki zao, wajibu na usawa, na kuwakumbusha watumishi hao kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma ikiwa ni apamoja na kutekeleza wajibu wao na kuahidi kuwachukulia hatua watakaokwenda kinyume.

“Nina imani kila mtumishi anafahamu vizuri majukumu yake, niwatake kila mmoja wenu kuyatekeleza kazi zenu kwa ufanisi, naahidi kutenda haki kwa kila mtumishi, sitamuonea mtu lakini sitasita kumchukulia hatua stahiki mtumishi asiotekeleza majukumu yake" amesema Mpume

Wakati huo huo Ofisa Mtendaji kata ya Mateves, Muyai Kivuyo,licha ya kumshukuru Mkurugenzi huyo, kwa kukaa pamoja na kujadili changamoto zinazowakabili, wamemuomba mkurugenzi huyo kuwapa taarifa za shughuli za miradi ambozo huendelea katima kata zao ili wafahamu na kushiriki katika kufuatilia miradi hiyo.

Kikao kazi hicho kimewakutanisha, watumishi wa ngazi za kata, ikiwemo maafisa watendaji kata, moafisa ugani na mifugo, maofisa maendeleo ya jamii, maofisa afya, maofisa elimu kata, pamoja na wakuu wa idara na vitengo.
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera  akiongea na watumishi Wa halmashauri yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...