Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekutana na Wadau wa Uchaguzi Mkoani Kagera na kutoa semina juu uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura.

Akizungumza na Wajumbe wa Mkutano huo mapema Septemba 23, Mwaka huu Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Asina Omari ametaja lengo la Semina hiyo kuwa ni kutoa taarifa juu ya kukamilika kwa maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura hivyo kuwaomba wadau hao kuwa mstari wa mbele kuhamasisha wananchi na jamii ili kufanikisha zoezi.

Bi Asina ameongeza kuwa mpaka sasa Tume imekamilisha sehemu kubwa ya maandalizi ya Uboreshaji ikiwa ni pamoja na uhakiki wa vituo vya kujiandikisha, uandikishaji wa majaribio, maandalizi ya Vifaa vya Uboreshaji wa Daftari, Mkakati wa Elimu ya mpiga kura, uzinduzi wa uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura n.k uboreshaji huo utafanyika kwa kutumia mashine  ya kielektroniki ya Biometriki (BVR).

Mkutano huo umehusisha Viongozi wa vyama Siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za kiraia, wawakilishi wa makundi maalum ya watu wenye Ulemavu, Vijana na wanawake na wanahabari.
 Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Asina Omari akitoa hotuba yake kwa wadau (hawapo pichani)  wa Uchaguzi Mkoani Kagera wakati akitoa taarifa juu ya kukamilika kwa maandalizi ya Daftari la kudumu la wapiga kura.
 Pichani ni Kaimu Mkurugenzi wa Daftari Bw. Frank Muhando akiwasilisha mada katika Mkutano na wadau wa Uchaguzi Mkoani Kagera.
Pichani ni Mwenyekiti wa Watu wenye ulemavu Mkoa wa Kagera SHIVYAWATA Bwn Novati Joseph akiuliza swali juu ya Kundi la watu wenye ulemavu kutopewa makabrasha yenye nukta nundu.

 Picha ya pamoja ya Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa wadau wa Uchaguzi Mkoani Kagera.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...