Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemsimamisha kwa muda Wakili wa kujitegemea Fatma Karume kufanya kazi za uwakili, baada ya upande wa Serikali kulalamikia matamshi aliyoyatoa katika kesi ya kikatiba ya kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi.

 Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu alifungua kesi ya kikatiba Mahakamani hapo akipinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi

Aidha Jaji Kiongozi Dkt, Eliezer Feleshi ameitupilia mbali maombi hayo ya Ado akisema kwamba, imemjumuisha Rais na kwa msimamo wa Mahakama Kuu kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.


Akitoa uamuzi huo, Jaji  Feleshi amesema amemsimamisha kwa muda Wakili Fatma kutokana na kuwasilisha hoja za maandishi ambazo zinaenda kinyume na maadili ya mawakili.


Pia Jaji Eliezer alisema ameitupilia mbali kesi hiyo kwa sababu  imemjumuisha Rais na kwa msimamo wa Mahakama Kuu kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.


Amesema, amekubaliana na baadhi ya sababu za kupinga maombi hayo zilizowasilishwa na upande wa serikali kwamba  kesi hiyo haina mashiko kwani inakiuka katiba.


Alisema kesi hiyo haina mashiko kwani inakiuka ibara ya 26(2) ya katiba na kwamba inakiuka kifungu cha sita cha sheria inayohusu masula ya Rais.


Hata hivyo, mahakama hiyo imezikataa hoja kwamba  hati ya kiapo inayounga mkono kesi ina mapungufu kwa kukiuka kifungu cha 19 kipengele cha tatu cha sheria ya mwenendo wa kesi za madai na kwamba hati ya kiapo inamapungufu.


Katika maombi ya msingi,  Shaibu anayewakilishwa na Wakili Karume

alikuwa anaiomba mahakama itamke rais ameshindwa kufuata misingi ya kazi yake kwa kufata Katiba kama  ilivyoainishwa katika ibara ya 26(1) kwa kumteua Adelardus Kilangi kuwa AG.

Pia alikua akiiomba mahakama itamke AG alishindwa kufuata matakwa ya katiba kwa kukubali kuwa AG kwa sababu kifungu hicho kinatamka kila mtu akiwemo Rais ana wajibu wa kufuata matakwa ya Katiba na AG anapaswa kufuata Katiba.


Anadai uteuzi wa AG uliofanyika 15/4/2018 unakiuka Katiba kwa mujibu wa kifungu hicho.


Anadai kwa mujibu wa ibara ya 59(1) inaeleza rais ana Mamlaka ya kumteua AG na  kwa mujibu wa ibara 59(2) AG atateuliwa miongoni mwa maafisa wenye sifa za kufanya kazi za wakili au watu wana sifa za kusajiliwa kuwa mawakili na wameshikilia sifa hizo kwa kipindi kisichopungua miaka 15.


Pia anadai AG hawajawahi kuwa afisa wa umma mwemye sifa za kufanya kazi za uwakili mfululizo kwa miaka 15.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...