Mwandishi wetu,Arusha 

Timu ya soka ya Kakoi ya wilaya ya Babati mkoa wa Manyara,imefanikiwa kuingia robo fainali katika michuano ya Chemchem CUP ambayo inafanyika wilayani Babati baada ya jana timu ya Kazamoyo kushindwa kutokea uwanjani . 

Katika michuano hiyo, ambayo inaendelea katika eneo la Mdori, jumla ya timu 20 za soka zinashiriki na timu nne za mpira wa pete ambapo kiasi cha sh 70 milioni zimetolewa na Taasisi ya uhifadhi ya Chemchem kuendesha michuano hiyo. Timu ya Kakoi amefanikiwa kutinga robo fainali baada ya kujipatia pointi tatu jana na kufanya kuongoza kundi lake, ambapo awali iliitandika timu ya Kona Mbaya magori 5-0. 

Wafungaji katika mchezo huo, walikuwa ni Devis Severine ambaye alifunga magori matatu , Shaban Jabu gori moja na Buzuka Amani gori moja. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Katibu wa michuano hiyo, Beno Alfred alisema michuano hiyo, inashirikisha jumla ya timu kutoka vijiji 10, ambavyo vinaunda jumuiya ya jamii ya uhifadhi ya wanyamapori ya Burunge. 

"katika michuano hiyo, kuna makundi manne ambapo timu mbili kutoka kila kundi zinasonga mbele kwa ajili ya kuingia robo fainali. Mratibu wa michuano hiyo wa Taasisi ya Chemchem ambayo imewekeza shughuli za kitalii katika hifadhi hiyo, Walter Pallanyo, alisema kiasi cha milioni 4.5 kinatarajiwa kutolewa kama zawadi kwa washindi. 

Pallangyo alisema timu zote ambazo zinashiriki, zilipewa jezi na mipira kwa ajili ya michuano hiyo ambayo hufanyika kila mwaka. "lengo la michuano hiyo ni kuwashirikisha vijana katika vita dhidi ya ujangili lakini pia kujua thamani ya uhifadhi wa maeneo yao kwa shughuli za kitalii"alisema 

Timu ya Manyara ndio ilitwaa ubingwa katika michuano ya Chemchem mwaka jana. Timu za mpira wa pete ambazo zinashiriki ni timu ya Mwada, Mdori, Walimu na Ngolei

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...