Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
MAMLAKA ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) imeandaa mkutano wa wadau wa bima ili utakaofanyika mkoani Mwanza mwezi huu ili kujadili maendeleo na changamoto zinazoikabili sekta hiyo, katika kipindi cha mwaka mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 12,2019 Kamishina wa TIRA, Tanzania  Dk. Mussa Juma amesema mkutano huo amao hufanyika kila mwaka mwezi huu wa tisa  safari hii mada kubwa itakuwa ni kuinua upenyo wa bima kwa kuongeza wigo wa bima kwa wasiokuwa na bima.

Aidha amesema mada hiyo inamalengo makuwa ya kutoa elimu ya bima kwa jamii na jukwaa kamili kwa ajili ya wadau wa Taasisi na kuongeza mtandao wa kibiashara  kitu kitakachoongeza malengo ya serikali ya awamu ya tano amayo imedhakia nchi kufikia kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Dk. Juma amesema, katika mkutano huo, unaotarajiwa kuanza septemba 24 hadi 29, mwaka huu, watakuwa pia watatoa elimu juu ya ufahamu wa bima, kubadirishana maarifa na utaalamu wa bima,kutoka kwa wataalamu wa ndani na nje ya nchi na pia katika wiki hiyo, taasisi ya bima itatoa jukwaa kamili na vifaa muhimu kwa maendeleo, uboreshaji wa maarifa ya ima na mazoezi.

“Katika wiki hiyo tutakuwa na matemezi ya bima, Utoaji Damu utoaji wa tunzo mbali mbali mbali za mwaka kwa washindo mbali mbali pamoja na michezo mbali mbali kiwamo mpira wa miguu na ama mikono”, amesema Dk. Juma

Amesema pia watajadili fursa na changamoto zinazoikabili sekta ya bima nchini pamoja na wajibu wa wasambazaji wa huduma hiyo ya bima.

"Katika mkutano huu Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashantu Kijaji anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, hii ni kwa sababu wizara yake ndio yenye dhamana ya usimamizi wa sekta ya fedha na bima ikiwemo, " amesema Dk. Juma.

Naye Katibu wa Taasisi ya Bima Tanzania, Ernest Kilumbi amesema wiki hiyo ya bima ni jukwaa sahihi kwa ajili ya kuanzisha na kuratibu shughuli za bima ikiwamo kutoa elimu, misaada kwa wazee, yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

"Wiki hii ya bima ni jukwaa kamili kabisa la kuwakutanisha wadau kwa lengo la kupeana taarifa na kuinua upenyo na kuuongeza kwa watu wasiokuwa na bima, " alisema.

Kwa upande wake Mwakilishi wa majaji katika utoaji tuzo za umahiri kwenye sekta ya Bima, Frenk Kitende amesema katika mkutano huo wa TIRA kwa kushirikiana na IIT imeona ni muhimu kuanzisha tuzo hizo ili kuweza kuwatambua na kuzawadi ufanisi kwenye uendeshaji, uongozi na utawala wa wadau katika sekta ya bima.

Amesema walipokea  jumla ya maombi 72 ya wadau kutoka taasisi mbali mbali za bima amapo kati ya hizo maombi 32 yalipitishwa huku 40 yakikataliwa kwa sababu mbalimbali.

"Majaji wote walifanya kazi kwa bidii kubwa kupitia maombi ya washiriki wote na kuhakiki taarifa ziluzowasilishwa, alama za ufaulu zitawekwa kwenye mtandao baada ya sherehe za utoaji tuzo zotakazofanyika Septemba 26 mwaka huu, " amesema. 

 Kamishana wa mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) Dk. Musa Juma akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkutano wa wadau mbali mbali wa bima unaotarajiwa kufanyika mkoani Mwanza kuanzia Septemba 24 hadi 29,2019. Mkutano huo umeandaliwa na TIRA kwa kushirikiana na Taasisi ya Bima Tanzania (IIT)  kwa lengo la kujadili maendeleo na changamoto zinazoikabili tasnia ya bima katika kipindi cha mwaka mmoja.
 Katibu wa Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) ,  Ernest Kilumbi, akizungumza katika mkutano huo

Mwakilishi wa majaji katika utoaji tuzo za umahiri katika sekta ya Bima,  Frenk Kitende akielezea namna wadau mbali mbali wa tasnia ya Bima watavyopewa tuzo ya kuweza kutambua na kuzawadi ufanisi kwenye uendeshaji, uongozi na utawala wa wadau katika sekta hiyo  katika mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...