Na mwandishi wetu, Arusha

WATOTO wa jamii ya wafugaji wa Lorkisalie Wilayani Monduli na Malambo Wilayani Ngorongoro wamenufaika kielimu baada ya kampuni ya ECLAT Foundation kujenga miundombinu ya madarasa ya shule zao za msingi kwa kutumia sh236 milioni. 

Ofisa miradi wa shirika lisilo la kiserikali la ECLAT Foundation, Bakiri Angalia aliyasema hayo wakati akielezea ujenzi wa miundombinu ya shule hizo mbili tofauti zilizopo kwenye jamii ya wafugaji. 

Angalia alisema kwenye shule ya msingi Lengijabe ya wilayani Monduli mkoani Arusha wametumia sh102 milioni kumalizia ujenzi wa madarasa sita. 

Alisema pia kwenye shule hiyo wametoa madawati 138, ujenzi wa matundu 16 ya vyoo na kuweka mfumo wa uvunaji maji ya mvua. Alisema kwenye ujenzi wa miundombinu ya shule ya msingi Malambo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wametumia sh134 milioni. 

"Tumejenga madarasa matatu na ofisi ya walimu, madawati 69 na kuweka mfumo wa nishati ya umeme wa jua," alisema Angalia. Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Monduli, Steven Ulaya akizungumza wakati akikabidhiwa madarasa ya shule hiyo aliipongeza ECLAT Foundation kwa kufanikisha ujenzi huo. 

Ulaya alisema wanaahidi kuhakikisha walimu, wanafunzi na jamii ya eneo hilo wanatunza miundombinu ya shule hiyo iliyofanikishwa na ECLAT Foundation. Mwenyekiti wa ECLAT Foundation, Peter Toima alisema wamekuwa wakisaidia jamii ya maeneo mbalimbali nchini katika kufanikisha maendeleo. 

"Tumefanikisha miradi mbalimbali nchini ikiwemo Monduli na Ngorongoro mkoani Arusha, Simanjiro mkoani Manyara, Tandahimba mkoani Mtwara na Kakonko mkoani Kigoma," alisema Toima. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha, Steven Ulaya akiwakabidhi hati ya kutambua mchango wao kwa jamii Mwenyekiti wa ECLAT Foundation, Peter Toima na Mkurugenzi wa Upendo Society Dkt Fred Heimbach.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha, Steven Ulaya (kushoto) kizungumza na wadau wa elimu, katikati ni Mwenyekiti wa ECLAT Foundation, Peter Toima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...