Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Hassan Juma Amour akitoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusu matumizi sahihi na salama ya Gesi ya kupikia huko Ofisi kwake Maisara Zanzibar. 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa katika mafunzo kuhusu matumizi sahihi na salama ya Gesi ya kupikia huko Ofisi za ZURA) Maisara Zanzibar.
Picha na Kijakazi Abdalla -Maelezo Zanzibar.


Na Kijakazi Abdalla,Maelezo 

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imewahakikishia wananchi kuwa gesi ya kupikia (LPG) ni nishati ambayo inazingatia misingi ya usalama ya kuepusha madhara ambayo yanaweza kutokea wakati wa matumizi.

Akitoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari huko Ofisini kwake Maisara Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar Hassan Juma Amour kuhusu matumizi sahihi na salama ya gesi ya kupikia amesema kuwa gesi ya kupikia (LGP) ni nishati rafiki wa mazingira.

Alisema kuwa gesi ya kupikia inapatikana baada ya kusafisha mafuta ghafi hivyo haina madhara kwani sasa watu wengi hupelekea kutumia nishati hiyo na kondokana na matumizi ya kuni ambayo yamekuwa yakiathiri mazingira.

Aidha alisema kuwa gesi husafirishwa na kuhifadhiwa kwenye mitungi kwa sababu ni rahisi kubadilishwa kwa hali ya kumiminika na kuzingatiwa viwango vinavyostahiki.

Hata hivyo Afisa Hassan alisema kuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma zilizo bora za gesi ya kupikia imewahakikishia kuwa inafanya ukaguzi kila maduka ambayo yanauza bidhaa hiyo kwa kuhakikisha wanakuwa na mizani iliyohakikiwa na Idara ya Mizani na vipimo Zanzibar.

Pia alisema inahakikisha kuwa mfanyabiashara huyo anakuwa na ujuzi wa kutumia bidhaa hiyo ili kuhakikisha pale linapotokea hitilafu anaweza kukabiliana nazo.Vilevile alisema aliwataka wasambazaji wa gesi ambao wanatumia usafiri kuhakikisha bidhaa hiyo inasafirishwa wima kwani ni hatari kusafirisha mitungi ya gesi ikiwa imelazwa.

“Tusizingatie faida tu tuzingatie usalama wetu kwani bidhaa hiyo ikisafirishwa ikiwa imelala huwa inajigonga gonga na kusababisha gesi kuvuja na kuleta madhara”alisema Hassan.Aidha alisema kuwa mitungi ya gesi inatakiwa kuteremshwa taratibu kutoka kwenye gari na watumiaji amewataka watumie katika sehemu zenye kutoa hewa na muangaza zaidi ili kuepusha madhara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...