Mfanyabiashara Yasin Katare, wa mbele mwenye tisheti nyekundu, anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, pamoja na aliyekuwa Mhasibu wa Takukuru, Godfrey Gugai wa nyuma mwenye tisheti ya mistari ya punda milia na wenzao wakitoka katika kizimba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya Yasin kukiri kosa na kuhukumiwa kulipa faini ya shilingi Milioni 100. Washtakiwa wengine wamekana makosa hayo

Ukiwa umepita muda takribabi wiki mbili tangu Rais John Magufuli atangaze kutoa ruhusa kwa washitakiwa wa kesi  za uhujumu uchumi kuomba msamaha na kukiri makosa yao, leo Oktoba 4, 2019 mshtakiwa mwenzie na aliyekuwa  Mhasibu Mkuu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai, Yasin Katare amehukumiwa kulipa faini ya Sh milioni 100 au kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kukiri mashitaka ya utakatishaji fedha.

Adhabu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
 Hata hivyo, kabla ya kusomwa kwa adhabu hiyo wakili wa utetezi, Shunde Mbutu aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu mshitakiwa kwa sababu ni kosa lake la kwanza na anafamilia inayomtegemea pia amedai mshitakiwa amekaa ndani mwaka wa pili na afya yake si nzuru kwani anaumwa na amekuwa akienda Hospitali ya Taifa Muhimbili kuhudhuria kliniki.

"Mshtakiwa hajaisumbua mahakama kwa kukiri kosa sambamba na msamaha wa rais kwa watu wanaopenda kukiri hivyo, aonewe huruma na kupewa adhabu ya faini ili kuungana na familia yake".

Hakimu Simba amemuhukumu mshitakiwa kulipa faini ya Sh milioni 100 kwa kuzingatia muda aliokaa gerezani muda mrefu  na ni mgonjwa hivyo, wakimpa adhabu kubwa itaendelea kutesa familia yake.

Pia ameswma, nyumba ya mshtakiwa itataifishwa na kuwa mali ya serikali na kwamba mshitakiwa akishindwa kulipa faini atatumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani.


Hatua ya Gugai na washitakiwa wenzake George Makaranga na  Leonard Aloys kugoma kuandika barua hiyo, imebainika  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati washitakiwa hao walipokuwa wakisomewa mashitaka upya baada ya mashitaka matatu kati 43 ya awali kuondolewa na hivyo kubaki na mashitaka 40 na  kati ya hayo 20 ni ya utakatishaji fedha na 19 ya kughushi ambapo baada ya kusomewa wamekana.


Katika mashitaka hayo mpya waliyosomewa  29 yanamkabili Gugai peke yake ikiwemo ya kupatikana na mali isiyo na maelezo ya Sh 3,634,961,105.02, huku hku Gugai na Makaranga wakishitakiwa kutakatisha fedha na Aloys na Gugai wanakabiliwa na mashitaka manane ikiwemo manne ya kughushi na manne ya utakatishaji fedha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...