Na Aalliyah Habib Rufiji Pwani

MKUU wa WIlaya ya Rufiji mkoani Pwani Juma Njwayo amewataka wananchi wilayani humo kuchagua viongozi watakaoweza kuwasaidia kuleta maendeleo badala ya kuchagua viongozi wanaochangia kuchochea migogoro ikiwemo ya wafugaji na wakulima huku viongozi hao wakijinufaisha kwa maslahi yao binafsi.

Ameyasema hayo wakati akihamasisha  uandikishaji wa daftari la wakazi kwa ajili ya kupiga kura kwa ajili ya  uchaguzi wa viongozi wa mitaa vitongoji na vijiji unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu nchi nzima.

"Msichague viongozi wanaoingiza ng'ombe usiku kwenye maeneo yenu huku nyie mnagombana wenzenu wanakusanya fedha wakati umefika wa kutowachagua viongozi hao chagueni wanoaweza kuwasaidia kuwaletea maendeleo yenu hiyo ndiyo dawa," alisema Njwayo.

Aliwakumbusha wananchi hao kuwa vitambulisho vya kupiga kura na vya utaifa havitatumika katika zoezi la kupiga kura na kuwataka kujitokeza kwasiku zilizobakia kujiandikisha kwakuwa hiyo nafasi pekee itakayomuwezesha kila mwananchi kupiga kura.

"Nawaambieni ndugu zangu msijidanganye vitambulisho hivyo havitatumika haviruhusiwi kisheria kajiandikisheni na nyie watendaji piteni nyumba hadi nyumba mashambani wafateni wananchi wajiandikishe ni haki yao kupiga kura," alisema Njwayo.

Awali Kamanda wa Takukuru Wilaya ya Rufiji Gwakisa Mwaikela aliwataka wagombea kuepuka vitendo vya rushwa katika uchaguzi na wananchi nao kukataa kupokea rushwa kwa kuwa sheria itachukua mkomdo wake.

"Chagueni viongozi watakaoweza kuwasaidia kuwaletea maendeleo msikubali kupewa zawadi wala kitu Chochote chenye kiashiria cha rushwa sheria itawabana haitaangalia nani ni nani,"alisema Gwakisa.

Baadhi ya Wananchi walisema mwitikio mdogo wa kijiandiksiha unatokana na baadhi ya wananchi kushinda mashambani na wengine kuishi maeneo ya mbali na kilipo vituo vya kujiandikisha hivyo kuona shida kama wanapoteza muda kwenda kujiandikishwa kwenyw daftari ka wakazi.
 Wananchi kijiji cha Muhoro wakimsikiliza Mkuu wao a Wilaya ya Rufiji Juma Njwayo pichani haonekani wakati akiwahamasisha kujitokeza kujiandikisha katika daftari.la orodha ya wakazi ili waweze kuliga kura kychagua vi0ngozi wa serikali za vijiji vyao na vitongoji Rufiji Mkoani Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani Juma Njwayo akitoa elimu kwa wananchi umuhimu wa kujiandikish katika daftari la orodha ya wakazi ili waweze kushiriki kupiga kura Nov 24 mwaka huu katika kijiji cha Mbwara Rufiji Mkoani Pwani akiwasisitizia kitambulisjo cha kupiga kura na uraia hakitaruhusiwa katika zoezi la upigaji kura.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...