Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, imeelezwa kuwa, mshtakiwa Erick Kabendera anakusudia kuanza majadiliano na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, (DPP) ya namna ya kumaliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili.

 Wakili anayemtetea Kabendera, Jebra Kambole ameeleza hayo leo Oktoba 11 Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile wakati kwaindhidi ya Kabendera ilipokuja kwa kutajwa

Mapema, wakili wa serikali Wankyo Simon alidai kuwa Kesi hiyo leo imepangwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado haujakamilika.

Baada ya Wankyo kueleza hayo, Wakili wa Kambole aliijulisha Mahakama taarifa hiyo kwa mujibu wa kifungu namba 194A(2) cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2019.

Baada ya taarifa hiyo kuelezwa, Wankyo alidai kuwa ni kweli jambo hilo limefanyika kuwa Kabendera ameandika barua na kwamba ipo Katika mchakato na kwamba watakapokuwa wamekamilisha wataitaarifu Mahakama.

 Baada ya kusikiliza hoja hizo Hakimu Rwizile ameahirisha Kesi hiyo hadi Oktoba 24, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Na kama kutakuwa na chochote kabla ya hiyo tarehe waiharifu Mahakama.

Kabendera ambaye ni mwandishi wa habari za ndani na nje, anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa zaidi ya sh 173 milioni.

Katika shtaka la kwanza ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho, Kabendera alijihusisha  na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Shtaka la pili ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho,bila ya sababu,alikwepa kodi ya sh. 173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Katika shtaka la tatu, kabendera anadaiwa kutakaisha Sh 173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na utakatishaji fedha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...