Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akijiandikisha kwenye Daftari la orodha ya Mpiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kituo cha Kujiandikisha Shule ya Msingi Kilimani iliyopo jijini Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kujiandikisha kwenye Daftari la orodha ya Mpiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kituo cha Kujiandikisha Shule ya Msingi Kilimani iliyopo jijini Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge,akitoa taarifa fupi kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani),ambaye alienda kujiandikisha kwenye Daftari la Orodha ya Mpiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kituo cha Kujiandikisha Shule ya Msingi Kilimani illiyopo jijini Dodoma.



Charles James, Michuzi TV

WATANZANIA wametakiwa kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la orodha ya wapiga kura ili waweze kupata nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan wakati alipoenda kujiandikisha katika daftari hilo kwenye Shule ya Kilimani jijini Dodoma leo.

Mama Samia amesema wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi bila kujali itikadi zao za vyama kujiandikisha lakini vile vile waweze kujitokeza kwa wingi kuchagua viongozi wanaowataka.

" Mimi leo nimeamua kutumia fursa hii kuja kujiandikisha katika mtaa wangu wa Salmini na najua ni haki yangu kuchagua Mwenyekiti wa Mtaa wangu na viongozi wangu kwa sababu najua makazi yangu hapo Dodoma na hawa ndio watakaosimamia mambo yangu kwenye mtaa wangu.

" Kwahiyo niwaombe sana ndugu zangu mtoke mkajiandikishe muweze kupiga kura lakini kubwa zaidi niwaombe wakati wa kuchagua mchague viongozi kweli watakaokwenda na kasi ya Serikali yetu, " Amesema Mama Samia.

Amewataka watanzania kuchagua viongozi waadilifu wenye kujali maslahi ya wananchi, wenye maadili ya kuwatumikia watanzania na wenye kutunza rasimali za wananchi wao na ambao watawasaidia viongozi wa ngazi za juu katika kuwatumikia watanzania.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Benelith Mahenge zoezi la uandikishaji ndani ya Mkoa huo limeanza jana na kwamba matarajio yao ni kuandikisha wananchi Laki Tisa.

" Idadi ya vituo ndani ya Mkoa wetu ni 3, 679 na toka jana tumeandikisha watu 156,000 hivyo tunaamini mpaka siku saba ziishe ambazo ni za uandikishaji tutakua tumezidi hata idadi kwa kuwa wananchi wengi pia wanaenda makazini hivyo siku za Jumamosi na Jumapili watapatikana kwa wingi," Amesema Dk Mahenge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...