Na Woinde shizza, Michuzi TV Arusha

SAKATA la wanandugu wa familia ya narehemu bilionea Erasto Msuya ambao ni wakazi wa Arusha wanaodaiwa kugombea mali  za marehemu Msuya limechukua sura mpya baada ya upande wa baba yake kuibuka na kudai hakuna mgogoro wa kugombea mali ila suala hilo linazushwa kwa maslahi ya upande wa mke wa marehemu.

Pia imekanusha madai ya kufunga nyumba tano za marehemu na kusababisha watoto kuishi hotelini na kudai kuwa mtoto mkubwa wa marehemu aitwaye  Kervin Msuya(22)aliamua kuishi mwenyewe hotelini kwa kupenda anasa zake na si kwa kufungiwa nyumba .

Akizungumza na vyombo vya habari, mama mzazi wa Marehemu Erasto, Ndeshu Msuya ameeleza bayana nyumba hizo zilifungwa kwa sababu ya usalama baada ya mke wa marehemu, Miriam Mrita kukamatwa kwa tuhuma za mauaji ya wifi i yake Anitha Msuya na kukosa mwangalizi kutoka na baadhi ya vitu kupotea ovyo.

Amesema hatua hiyo ilikuja kutokana na fnyumba aliyokuwa akiishi marehemu na familia yake ,upande wa mke wa marehemu kutaka kuiuza kwa kuwa haikuwa sehemu ya mali za mirathi za marehemu zilizokuwa zimeorodheshwa.

Mama Ndeshu alidai kwamba  funguo za myumba hizo zilikabidhiwa kwa ndugu hao wa Mke ambao hadi sasa bado wanazo.

Amefafanua Kervin ambaye ni mtoto mkubwa wa marehemu alikuwa akisoma nje ya nchi nchini Australia lakini walimrejesha nyumbani bila kumaliza masomo yake ili kumtumia kama mtaji wa kufuatilia mali za marehemu baba yake.

Mama huyo amedai anasikitishwa na hatua ya watoto wa marehemu wapatao wanne kutopewa haki ya mgao wa mali za marehemu baba yao kwani kwa sasa mali hizo zinawanufaisha ndugu wa uoande wa mke ambao wamejigawia kusimamia.

"Sisi kama wazazi wa marehemu tunasikitishwa sana kumtumia huyu kijana suala la mali ,kwanza wamemkatisha masomo yake na pale hotelini hana mamlaka yoyote zaidi ya kutumwa kwenye kununua vitu vya hotelini sokoni,"amesema Mama.

Hata hivyo amedai hakuna ubishi kuwa marehemu Erasto Msuya aliuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya 20 katika eneo la Mijohoroni wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, Agosti 7mwaka 2013. Kifo cha marehemu ambaye alikuwa mfanyabiashara wa Madini ya Tanzanite kiliacha simanzi

Imeelezwa kuwa katika maisha yake Erasto alifanikiwa kuwa na mali mbalimbali ikiwemo vitega uchumi kadhaa magari ya kifahari,nyumba za kisasa ,mashamba makubwa ,migodi na hoteli.

Mama mzazi wa Marehemu Erasto Msuya,Ndeshu  Msuya anaeleza jinsi Mke wa marehemu Miriam Mrita jinsi alivyoweka pembeni ubinadamu na kuanza kuuza chap chap baadhi ya mali za marehemu mumewe kabla hata ya mazishi ikiwemo kuhamisha mali mbalimbali na kupeleka kusikojulikana, kubadilisha mikataba ya umiliki wa mali na  kuandika jina lake.

"Nashukuru waandishi wa habari kwa kuingilia kati jambo hili naimani nchi itaelewa ukweli .Mkuu wa Wilaya (Jerry Muro)Erasto alikuwa mtoto  wangu pekee wa kiume kwenye uzao wangu kati ya watoto saba  wakiwemo mabinti saba,mtoto wangu aliuawa Mijohoroni kila mtu anajua kwamba alipigwa risasi nyingi.

"Kilichotokea muda mfupi  baada ya kijana wangu kuuawa mke wake(Miriam) huku ndani alianza kutoa vitu vyote kwenye Selfu  zikiwemo fedha na document mbalimbali na kupeleka kusikojulikana.

"Aliondoka na kwenda kuvunja ofisi ya marehemu na kuchukua documents zote yakiwemo Madini na fedha,hamuwezi kuamini kuwa  Erasto alikuwa bilionea, mfanyabiashara wa Madini lakini hatukuona hata sample chafu ya Madini ya Tanzanite yanayomhusu Erasto labda ungesema alikuwa muuza Maandazi.

"Baada ya kuzika kijana wetu tulikaa kikao cha ukoo pale Boma,tukamuuliza Mwali(Miriam) utaolewa ama unabaki kwenye boma ,akasema atabaki kwenye boma(Nyumbani kwa Marehemu),"amesema.

Ameongeza kikao cha ukoo kilikaa na kuorozesha mali zote za marehemu kwa kuziona na kuelezwa, wakaviweka kwenye mirathi na kumwandikia Miriam, kwamba asimamie mji wako kama ambavyo mlikuwa mkiendesha mji na Mume wako.

Pia amesema baadaye kabla yakuzika wakaambiwa kuwa  baadhi ya vitu yakiwemo mabegi yamesombwa usiku wa manane na Gari aina ya Rand cruise na kupelekwa kusikojulikana.

"Ndipo tulipojua huyu mwanamke ni mpumbavu hata Bibilia inasema mwanamke mpumbavu huvunja mji wake mwenyewe uliona wapi mali zako halafu unajiibia mwenyewe ,lakini hatukutaka kumuuliza chochote.

"Baada ya kukabidhiwa kama msimamizi wa mirathi alianza mizengwe akidai ni wakati wake wa kula good time(Kula raha) ,alianza kujigawa na kukata mawasiliano na sisi ,alianza kuuza vitu ikiwemo viwanja huko Njiro ,Magari na kubadilisha majina na kuandika Miriam Stephano Mrita.

"Tulimchagua Miriam kama msimamizi wa mirathi ili akusanye na kama kuna madeni alipe na baadae agawe mali kwa watoto wake wanne na yeye mwenyewe, lakini akaona kama amechaguliwa kuwa mmiliki wa Mali na kufanya atakavyo ,"amedai.

Ameongeza fedha zilizopo kwenye akaunti mbalimbali za marehemu kwenye mabenki ,Marehemu aliacha maelezo ya maandishi  kuwa iwapo atafariki dunia wazazi wake wakiwa bado hai,asilimia 40 wagawane wazazi pamoja na Dada zangu na  asilimia 60 ibaki kwenye akaunti kwa ajili ya mke wake  na watoto.

Amesema wao kama wazazi wanaona dariri mbaya za watoto wa marehemu kukosa haki yao ndio maana wameingilia kati jambo hili na si kwa kutaka mali za Marehemu kijana wetu bali tunataka Mali ya Marehemu igawanywe kwa watoto

Kwa upande wake Bahati Msuya ambaye ni dada wa marehemu amesema kuwa wao kama ndugu wa marehemu hawana nia ya kugombea mali za marehemu kaka yao isipokuwa wanachotaka ni watoto wa marehemu wapewe haki ya kumiliki Mali za Marehemu baba yao.

Amesema mtoto wa marehemu aitwaye Glory  Msuya ambaye yupo masomoni nchini  Canada ameshindwa kuendelea na masomo yake ya elimu ya juu baada ya ndugu wa mama yake wanaosimamia hoteli na miradi mingine kukataa kumlipia ada wakimtaka arejee nchini.

Awali mtoto mkubwa wa Marehemu,Kervin Msuya alilalamikia ndugu wa upande wa baba yake kutaka kumpora Mali za baba yake na kumfungua nyumba ya marehemu baba yake jambo ambalo lilimfanya akose makazi na kulala hotelini .

Hata hivyo suala hilo lilitatuliwa na Mkuu wa wilaya Jerry Muro kwa kuamuru kijana huyo nanwenzake  kurejea katika nyumba hiyo ili kuendelea na makazi .

Muro aliagiza pande zote zinazozozana kufika ofisini kwake kesho jumatatu SAA nne asubuhi  ili kufikia mwafaka wa changamoto zilizojitokeza.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...