Na Ripota Wetu- GEITA
Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 20 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa ukumbi wa chakula katika shule ya Sekondari ya Shantamine.
Amesema ataitoa fedha hiyo kwa ajili ya kupunguza adha kwa wanafunzi wa shule hiyo wanaolazimika kukaa nje wakati wa kula chakula hasa katika kipindi cha mvua.
Ahadi hiyo ameitoa leo mkoani Geita wakati alipokuwa akizungumza na jumla ya Wahitimu 263 wa kidato cha nne kwenye mahafali yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Shantamine.
Ombi hilo linakuja kufuatia risala iliyosomwa kwake na Wahitimu wa kidato cha nne wakiomba kukamilishiwa ujenzi wa ukumbi huo utakaoweza kuwahudumia wanafunzi wengi kutokana na idadi yao kuongezeka hali inayowalazimu kupata shida wakati mvua ikiwa inanyesha
Katika hatua nyingine, Mhe. Kanyasu ameahidi kuchimba kisima kirefu zaidi katika shule hiyo kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa kike wanaolazimika kutoka nje ya shule kutafuta maji
Ameeleza kuwa maombi kwa ajili ya uchimbaji wa kisima hicho yamewashawasilishwa katika wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na wanachosubili ni utaratibu wa namna ya kukichimba kisima hicho.
Hata hivyo Mhe. Kanyasu ameeleza kuwa jumla ya visima viwili vilishachimbwa katika shule hiyo lakini ilibainika kuwa havina maji na eneo hilo lilionekana kuwa maji yake yana chumvi sana.
Akizungumzia kuhusu ombi la kupatiwa umeme katika shule hiyo, Mhe. Kanyasu amesema ifikapo mwezi mei mwakani shule hiyo itakuwa tayari ina umeme.
Aidha, Mhe. Kanyasu amewaahidi wanafunzi wa shule hiyo kuwa atashirikiana na madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Geita kujenga mabweni kadiri pesa inavyojitokeza ili kuwanusuru wanafunzi wanaolazimika kupanga nyumba nje ya shule hali inayopelekea wanafunzi wengi wa kike kuacha masomo baada ya kupata mimba.
Mbali na hilo, Mhe. Kanyasu amewatakia heri wahitimu hao katika mitihani yao na kuwataka wasiridhikena elimu hiyo na badala yake wajiendeleze zaidi
Naye. Diwani wa Kata ya Mtakuja. Constantine Morandi amewataka wananfunzi hao wajiandae kikamilifu katika mitihani ya kuhitimukidato cha nne ili kuweza kuileta sifa shule hiyo.
‘’Nina washukuru wazazi pamoja na waalimu kwa ushirikiano wenu katika kuhakikisha wanafunzi 263 wanahitimu masomo yao’
Akizungumza mhitimu wa kidato cha nne kwa niaba ya wenzake , Anna Masumbuko amesema wapo tayari kwa ajili ya mtihani wa mwisho na wanategemea kufaulu vizuri katika mitihani yao.
Baadhi ya Wahitimu wa kidato cha nne wakituimbiza wimbo wa kuwaaga wanafunzi wenzoa katika mahafali yao yaliyofanyika katika shule ya Sekondari ya Shantamine Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimkabidhi cheti mwanafunzi bora, Editha Karlo aliyekuwa akiongoza masomo kwa jumla ya Wahitimu 263 wa kidato cha nne wakati wa mahafali yaliyofanyika leo katika shule ya Sekondari ya Shantamine iliyoko mkoani Geita
Diwani wa kata ya Mtakuja, Constantine Morandi akizungumza na wahitimu wa kidato cha nne kabla ya Mbunge wa Geita Mjini, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne wapatao 263 Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimkabidhi cheti mwanafunzi bora kwa masomo ya Sayansi, Elinami Habakuki wakati wa mahafali ya kidato cha nne kwa jumla Wahitimu 263 yaliyofanyika leo katika shule ya Sekondari ya Shantamine iliyoko mkoani Geita
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Shantamine wakiwa wameshika jezi za michezo kwa ajili ya wanafunzi wa kike na kiume ambayo ni zawadi walizokabidhiwa na Mbunge huyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...