Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAKALA wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi(OSHA)umezitaka kampuni za mafuta na gesi ambazo ziko nchini kuhakikisha zinasajiliwa na wakala huo kwa lengo la kuhakikisha zinafanya shughuli zao katika mazingira yaliyo salama kwa viwanda na nchi kwa ujumla.

Akizungumza leo Oktoba 2,2019 katika kongamano la tatu la wadau wa mafuta na gesi lililoanza leo jijini Dar es Salaam Mkaguzi wa Usalama wa Mifumo ya Umeme kutoka OSHA Mhandisi Maria Ndasikoy amesema tunapsema Tanzania iko kwenye uchumi wa viwanda lazima viwanda hivyo viwe salama wakati wote.

"Tupo kwenye kongamano hili la wadau wa mafuta na gesi kwa ajili ya kuwaeleza umuhimu wa kujisajili OSHA.Lazima kampuni au kiwanda kinachojihusisha na gesi na mafuta ziwe salama wakati wote.

"Tunafahamu katika shughuli za gesi na mafuta kuna vihatarishi vingi na kwa maana hiyo OSHA lazima tusimame imara kwa kusimamia majukumu yetu kikamilifu,"amesema Mhandisi Ndasikoy.

Ameongeza kwa kampuni za mafuta na gesi ambazo hazijasajiliwa watatumia nafasi hiyo kuzisajili na baada ya hapo watakwenda kukagua kwa kutumia vifaa malumu walivyonavyo ili kuangalia usalama kuanzia wa wafanyakazi, kiwanda chenyewe na usalama wa nchi kwa ujumla.

"Kwa kutumia vifaa vyetu tunaweza kukagua kiwanda cha gesi na gesi yenyewe kwa hatua mbalimbali.Pia kwa kutumia vifaa vyetu lazima tukague na mfumo wa umeme maana kama kutakuwa na tatizo ni rahisi kiwanda kuungua na kuleta madhara kwa Watanzania,"amesema.

Ameongeza OSHA ni jukumu lao pia kuangalia mazingira kwa wafanyakazi , hivyo kama gesi inavuja inaweza kuleta athari kwa mfanyakazi na uharibu wa mazingira.

"Hivyo wakati mkakati wa nchi yetu ni kuelekea Tanzania ya viwanda ili kufikia uchumi wa kati maana yake lazima twende huko tukiwa salama,"amesema Mhandisi Ndasikoy.

Kuhusu hali ilivyo kwa sasa amesema kuna muamko mkubwa sana kwani wawekezaji wengi wamejisajili OSHA na wao wanakwenda kuwakagua. Hata hivyo ametoa rai kwa kampuni zinazokuja nchini kuwekeza katika gesi na mafuta ni vema zikahakikisha zinajisajili OSHA.

"Wakumbuke kufika katika ofisi zetu kujisajili ili watambulike wao wa akina nani na wanatumia vifaa gani katika kampuni zao.Wakikaguliwa itakuwa rasihi kukabiliana na madhara ambayo yanaweza kujitokeza.Pia TIC kuna ofisi zetu za OSHA, hivyo wanaweza kwenda hapo kujisajili,"amesema.
 Mmoja ya wadau akitoa maoni yake baada ya kutembelea banda la OSHA lililopo kwenye kongamano la tatu la wadau wa mafuta na gesi lililoanza Leo jijini Dar es Salaam
 Mkaguzi wa Usalama wa Mifumo ya  Umeme kutoka OSHA Mhandisi Maria Ndasikoy akimsikiliza mmoja ya wadau wa mafuta na gesi ambao wapo kwenye kongamano la tatu la wadau wa mafuta na gesi linaloendelea jijini Dar es Salaam
Mkaguzi wa Usalama wa Mifumo ya Umeme kutoka OSHA akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salam wakati anatoa rai kwa kampuni za gesi na mafuta ambazo bado hazijasajiliwa OSHA kuhakikisha zinajisajili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...