Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamgamba John Kabudi (Mb) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Amina Mohammed katika ofisi za Umoja huo New York Marekani
 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Amina Mohammed akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) hayupo pichani, wakati akimkaribisha katika ofisi za Umoja huo zilizopo New York Marekani
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Amina Mohammed (Hayupo pichani) wakati alipokwenda katika ofisi za Umoja wa Mataifa zilizopo New York Marekani
 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Amina Mohammed na baadhi ya wajumbe wake wakiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi na wajumbe wake (hawapo pichani) katika ofisi za Umoja wa Mataifa zilizopo New York Marekani.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Amina Mohammed na wajumbe wake wakiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na ujumbe wake. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizopo New York,Marekani.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Amina Mohammed ameisihi Tanzania kuendelea kuimarisha amani katika ukanda wa maziwa makuu pamoja na kuendelea kuchangia kutoa askari wa vikosi vya ulinzi wa amani duniani.

Naibu Katibu Mkuu Dkt. Amina Mohammed ametoa wito huo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiorikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) Jijini New York nchini Marekani na kuongeza kuwa Umoja wa Mataifa unatambua mchango wa Tanzania katika ulinzi wa amani duniani na kwamba Umoja huo uko tayari kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza jitihada hizo ili kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi.

“Tanzania imekuwa muhimili muhimu katika kuhimiza amani katika ukanda wa maziwa makuu ikiwa ni pamoja na kuhifadhi wakimbizi kutoka ukanda huo kwa miaka mingi bila kuchoka” alisema Dkt. Amina

Kwa upande wake waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema kuwa Tanzania inatambua nafasi ya Umoja wa Mataifa na kwamba itasalia kuwa mwanachama wa umoja huo.
“Napenda kukuhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kutoa askari wake katika vikosi vya ulinzi wa amani katika maeneo mbalimbali duniani,” alisema Prof. Kabudi

Waziri Kabudi aliendelea kumueleza Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hatua mbalimbali ambazo Tanzania imepiga katika masuala ya maendeleo endelevu (SDGs) ikiwa ni pamoja na afya,maji, ushirikishwaji wa wanawake katika maamuzi pamoja na masuala ya kuimarika kwa demokrasia nchini.

Prof. Kabudi amehitimisha ziara yake ya kikazi nchini Marekani alipokuwa akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...