Na woinde shizza Michuzi Tv, Arusha 

Naibu waziri wa mifugo na uvuvi ABDALLAH ULEGA Amewataka wafugaji na wafanya biashara wa mifugo  kuunga mkono uuzaji ng’ombe kwa kilo na kuondokana na uuzaji mifugo kwa makisio, kwani litaleta thamani kwa mifugo pia maendeleo kwa mfugaji  na tija kwa serikali kuweza kukusanya mapato yake  

Akizungumza na wafugaji pamoja na wafanya biashara wakati akifunga mafunzo ya elimu kwa mfugaji na mfanya biashara juu ya uuzaji ng’ombe kwa kutumia mizani wilayani longido Mkoani Arusha  Naibu waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah ulega amesema Minada yote nchi nzima lazima ng’ombe auzwe kwa kilo ili kuwe na kiwango maalumu cha uuzaji wa ng’ombe

 ULEGA   Amesema mfanya biashara yeyote atakaebainika kuhusika  kununua au kuuza mifugo nje ya eneo lilotengwa kwa ajili ya uuzaji na ununuzi wa mifugo [MINADA] watachukuliwa hatua kali za kisheria na kuwaita wahujumu uchumi 

"mtu yeyote mfugaji ambaye atakutwa anauza Mifugo nje ya Mnada tutamchukulia hatua kali na siokulipa faini tu bali tutampeleka Mahakamani na tutamfungulia kesi ya uhujumu uchumi "alisema Ulega

ULEGA Akiwa katika moja ya viwanda vya kusindika maziwa kijulikanacho kwa jina la Kilimanjaro Freshi  Amesema ameridhishwa na uendeshaji wa kiwanda hicho kwa kununua maziwa kwa wafugaji wadogo wadogo na kuanzisha kitengo maalumu cha   kutoa  elimu kwa wafugaji  jinsi gani ya kuweza kuwapa chakula bora ili waweze kutoa maziwa ya kutosha

 Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Longido Jumaa Muhina Aliwataka wafugaji hao  kuachana na dhana yakufuga Mifugo mingi ambayo awanatija badala yake wafuge mifugo michache yenye tija

"nibora mfuge Mifugo mitatu au miwili yenye tija kuliko kufuga lundo la Mifugo ambayo aina faida yeyote, unakuta mtu anamifugo rundo na mungine ana mmoja lakini unakuta ukipima kwenye mizani unakuta uzito nisawa sasa sasahivi fugeni mifugo michache yenye tija "Alisema Muhina

Mmoja wa Mfugaji huyo aliyetambulika kwa jina la  Olisienda Sadalla alishukuru kwa mafunzo aliyoyapata na kuhaidi kuwa watafuata sheria na kanuni zote zinazotakiwa na serikali ili wasiingie kwenye matatizo. 
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi nchini Tanzania, Abdallah Ulega akizungumza na wafugaji na wafanya biashara wa wilaya ya Longido (hawapo Pichani) wakati alipokuwa Kufuga mafunzo ya siku moja walikuwa wakifanya katika ukumbi wa St. Theresia uliopo Namanga mkoani Arusha, ambapo aliwataka wafugaji hao kutotorosha mifugo na kwenda kuuza nje ya nchi badala yake wafaate sheria na kanuni huku akibainisha kuwa atakae Kusuka hatua kali itachukuliwa dhidi yake ikiwepokufugwa(picha na woinde shizza, Arusha). 


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Tanzania Abdallah Ulega akionja maziwawyanatengenezwa na kamanda cha KILIMANJARO Fresh wakati alipotembelea Kiwanda hicho kuangalia namna kinavyofanya kazi(picha na Woinde shizza ,Arusha.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi nchini Tanzania, Abdallah Ulega akikagua maziwa aina ya Kilimanjaro Freshi yanayotengenezwa na kiwanda  cha  KILIMANJARO Fresh wakati alipofanya ziara yakutembelea  kiwanda hicho jana kilichopo Ndani ya halmashauri ya jiji la  Arusha ambapo aliwasihi watanzania kupenda kutumia vyakwao na sio bidhaa za nje ya Nchi (picha na Woinde shizza, Arusha). 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...