Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akijadiliana mambo mbalimbali na Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) walipokutana katika Mji wa Sandton, Johannersburg, Afrika Kusini, Kando ya Kongamano kubwa la Pili la Jukwaa la Uwekezaji lililoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, ambapo Benki hiyo imeahidi kuipatia mikopo zaidi Tanzania.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akijadiliana mambo mbalimbali na Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) walipokutana katika Mji wa Sandton, Johannesburg, Afrika Kusini, Kando ya Kongamano kubwa la Pili la Jukwaa la Uwekezaji lililoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, ambapo Benki hiyo imeahidi kuipatia mikopo zaidi Tanzania.
Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) akimsikiliza kwa makini Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), walipokutana na kufanya mazungumzo katika Mji wa Sandton, Johannersburg, Afrika Kusini, Kando ya Kongamano kubwa la Pili la Jukwaa la Uwekezaji lililoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, ambapo Benki hiyo imeahidi kuipatia mikopo zaidi Tanzania.(Picha na Wizara ya Fedha na Mipango-Johannesburg)





Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akisalimiana na Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) walipokutana na kufanya mazungumzo katika Mji wa Sandton, Johannesburg, Afrika Kusini, Kando ya Kongamano kubwa la Pili la Jukwaa la Uwekezaji lililoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akiagana na Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) baada ya kumaliza mazungumzo yao katika Mji wa Sandton, Johannesburg, Afrika Kusini, Kando ya Kongamano kubwa la Pili la Jukwaa la Uwekezaji lililoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, ambapo Benki hiyo imeahidi kuipatia mikopo nafuu zaidi Tanzania kuanzia mwakani
…………………….

Na Benny Mwaipaja, Johannesburg

WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini wa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse, ambapo Benki hiyo imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 200 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mazungumzo ya viongozi hao yamefanyika katika Mji wa Sandton, Johannesburg nchini Afrika Kusini, kando ya Kongamano la Pili la Jukwaa la Uwekezaji Afrika lililoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB.

Dkt Mpango amesema kuwa Benki hiyo imekuwa mbia mzuri wa Tanzania ambapo mwaka huu pekee imetoa mkopo wa dola bilioni 1 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na imeahidi kutoa kiasi kingine cha dola milioni 200 baada ya Bodi ya Benki hiyo kukutana mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu kwa ajili kuidhinisha mkopo huo

Alisema kuwa amemwalika Rais huyo wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Bw. Tadesse, kufanya ziara ya kikazi nchini Tanzania hivi karibuni ili kujionea miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ukiwemo mradi wa kuzalisha umeme wa Kilwa pamoja na miradi mingine ambayo Benki hiyo inaweza kutoa mkopo

Kwa upande wake, Rais wa TDB Bw. Admassu Tadesse amesifu uhusiano imara uliopo kati ya Benki yake na Serikali ya Tanzania na kuahidi kuwa Benki hiyo itahakikisha inashirikiana nayo kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya wananchi wake.

“Tumekuwa na mjadala mzuri na Mhesimiwa Dkt. Mpango na Benki yetu imekuwa mshirika mzuri wa maendeleo ya Tanzania katika kipindi cha miaka michache iliyopita kwenye yyanja za nishati ya umeme na miundombinu ya usafirishaji” alisema Bw. Tadesse

Alisema kuwa mwaka huu Benki yake kwa kushirikiana na washirika wake wengine ambao ni taasisi za kibenki imeongeza mtaji wa dola milioni 500 hatua iliyoijengea Benki yake uwezo wa kutoa mikopo zaidi ambapo mwakani itaipatia mikopo kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya kimkakati ya miundombinu itakayokuwa na umuhimu mkubwa si tu kwa Tanzania, bali pia kikanda.

Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) ilianzishwa mwaka 1985 ikiwa na mali zenye thamani ya dola za Marekani bilioni 5.6 ambapo lengo lake kubwa ni kutoa mikopo inayochochea miradi inayochochea ukuaji wa biashara, ikiwemo miundombinu, utangamano wa kiuchumi na ushauri wa kibiashara kwa nchi wanachama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...