Jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga likiwa katika ukarabati Mkubwa unaoendelea.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (kushoto) akikagua ukarabati Mkubwa wa Jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Sumbawanga.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Sumbawanga Mhe. David Mrango (wa pili kushoto) akiongozana na Jaji Mkuu kukagua ukarabati mkubwa wa Jengo la Mahakama Kuu Sumbawanga. Kulia ni Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Leonard Magacha akifuatiwa na Mtendaji wa Kanda ya Sumbawanga, Emmanuel Munda.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (kushoto) akikagua shughuli za Mahakama katika Mahakama ya Mwanzo Sumbawanga mjini. kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Sumbawanga Mhe. David Mrango na katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Tehama wa Mahakama ya Tanzania, Machumu Essaba.
Jengo la Mahakama ya Mwanzo Laela lililopo Sumbawanga mkoani Rukwa.

***********************************

Lydia Churi-Mahakama, Sumbawanga

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Majaji, NaibuWasajili, Watendaji na Mahakimu wote nchini kutumia mamlaka yao ya usimamizi kuhakikisha wanakagua mfumo wa kusajili na kuratibu mashauri (JSDS II) ili kuona namna mashauri yanavyosajiliwa na kurekebisha endapo kuna makosa. Jaji Mkuu ametoa agizo hilo kufuatia hatua ya Mahakama ya Tanzania ya kuamu akufanya shughuli zake kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na kutaka kuacha kupokea takwimu zake kwa njia ya makaratasi na badala yake, itakuwa ikizisoma takwimu hizo kwa njia ya mtandao.

“Mwaka huu utakuwa ni mwaka wa mwisho kwa Mahakama kupokea takwimukwenye makaratasi, tutakuwa tukizisoma moja kwa moja kwenye mtandao”,alisema Jaji Mkuu alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari wakatiakifanya majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu katika mikoa ya Songwe na Rukwa.

“Lengo ni kwenda katika Mahakama ya karne ya 21, Mahakama inayotegemeazaidi mtandao kuliko kutegemea makaratasi”, alisema.
Alisema mfumo wa kusajili na kuratibu mashauri utawawezesha viongozi wa
Mahakama kujua ni mashauri mangapi yamesajiliwa nchini, mangapi
hayajapangiwa Majaji na Mahakimu, na mangapi yamezidi muda wa kuwepoMahakamani na hivyo kufuatilia kwa urahisi.

Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, mfumo wa JSDS II utasaidia kuzidisha uwazi katikashughuli za Mahakama na kuongeza imani zaidi ya wananchi kwa Mhimili huo.

Alisema Mahakama imedhamiria kuingia katika Tehama ambapo mwezi
Julai mwaka huu iliingia Mkataba wenye thamani ya Sh. bilioni 4.1 na
Shirika la Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL) utakaowezesha
Mahakama kuingizwa kwenye Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ambapo
majengo 157 ya Mahakama nchini yataunganishwa. 

Mkataba huo utawezesha kuunganishwa kwa majengo ya Mahakama
kuanzia Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu, Mahakama za Hakimu
Mkazi, Mahakama za Wilaya na baadhi ya Mahakama za Mwanzo zenye
majengo ya kisasa. Mahakama zitakazounganishwa kwenye mtandao huo ni Mahakama ya Rufani 1, Mahakama Kuu 16, Mahakama Kuu Maalumu
(Specialized Division 4, Mahakama za Mkoa 29, Mahakama za Wilaya 112
na Mahakama za Mwanzo 10.

Alizitaja faida za Mahakama kusajili mashauri kwa njia ya mtandao kuwa ni
pamoja na kuwasaidia mwananchi mwenye shauri Mahakama kufahamu
mwenendo mzima wa shauri kwa kujua kila hatua ya shauri lake kwa kufahamuhatua zinazofuata kwenye shauri lake kupitia mtandao.

Jaji Mkuu amehitimisha ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Songwe na Rukwaambapo alikagua shughuli mbalimbali za Mahakama ikiwemo miradi ya ujenzi wa majengo ya mahakama na hali ya utoaji haki kwa ujumla. Katika ziara hiyo, Jaji Mkuu alikagua ujenzi wa majengo ya Mahakama za Mwanzo za Mlowo mkoani Songwe na Mahakama za Mwanzo za Msanzi na Laela mkoani Rukwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...