Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Bw. Masanja Kungu Kadogosa akizungumza na waandishi wa habari wakati mawaziri wa mambo ya Nje wa nchi za NORDIC na Afrika wakipotembelea kujionea ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Umeme SGR eneo la Vingunguti Kiembembuzi leo.
Mmoja wa mawaziri hao akizungumza mara baada ya kutembelea mradi huo.
Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka nchi za Nordic na Afrika watembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro, kuanzia Stesheni ya Dar es Salaam hadi Vingunguti jijini Dar es Salaam Novemba 09, 2019.

Baadhi ya Mawaziri wa mambo ya Nje wa Nchi za Afrika walioshiriki Mkutano wa 18 wa NORDIC wamefanya ziara kujionea maendeleo ya Ujenzi wa Reli ya kisasa unaoendelea ambao umefikia asilimia 71 hadi kukamilika kwake huku matarajio ya kufanyika kwa majaribio ya awali kutoka Dar Es Salaam hadi Morogoro yakitarajiwa kufanywa Mwezi April,2019.

Wakizungumza baada ya kufanya ziara ya kujionea ujenzi huo kuanzia eneo la Stesheni hadi Vingunguti jijini Dar es Salaam baadhi ya mawaziri hao akiwemo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Balozi Abou Bakr Hefny amesema ujenzi huo ni kielelezo kikubwa cha maendeleo kwa Taifa lolote lile kutokana na ukweli kuwa uwekezaji ambao unahitajika kwa jamii yeyote inayohitaji maendeleo ya haraka ya watu wake.

Kwa upande wake waziri wa mambo ya Nje wa Nigeria Mhe Zubairu DaDa amesema katika nchi za Afrika baadhi ya wanasiasa hukosoa kitendo cha Nchi kukopa ili kuwekeza katika miundo mbinu na kuongeza kuwa iwe Nchi inakopa au inatumia hela zake za ndani na kuwekeza katika miradi inayogusa watu na maendeleo yao kama ilivyo katika ujenzi wa Reli ya Kisasa ni jambo la kuigwa na la kuungwa mkono na wala si jambo la kubeza hata kidogo.

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la reli Tanzania Bwana Masanja Kadogosa amesema mpaka sasa ujenzi wa reli hiyo umefikia asilimia 71 na kwamba mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa zinasababisha changamoto ya kuendelea na kazi kwa kasi kubwa na kubainisha kuwa mwezi April mwaka 2019 kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro kitakuwa kimekamilika na kile cha Morogoro hadi Dodoma kikitarajiwa kukamilika mwaka 2021.

Kwa upande wake Mkuu wa Itifaki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert Ibuge amesema kikao cha NORDIC kilikuwa kikihusu maendeleo yanayogusa watu ambapo kati ya mambo yanayogusa watu wengi ni uchukuzi na usafirishaji jambo lililomlazimu kuwatembeza baadhi ya mawaziri walioshiriki mkutano huo katika mradi huo wa ujenzi wa reli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...