Mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya Misafi George Misafi amewataka vijana nchini kufanya kazi zenye tija kwa ajili ya kumsaidia Rais Dkt John Magufuli kujenga uchumi wa Taifa kwa kutumia raslimali za Taifa badala ya vijana kushinda vijiweni pasipo kufanya kazi.

Akizungumza jana wakati akiwakabidhi kiasi cha shilingi 500,000 za kununua vifaa vya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) kata ya Makorongini mjini Iringa ,Misafi alisema kuwa jukumu kubwa la vijana ni kufanya kazi zenye tija ya kiuchumi ili kusaidia kulipeleka Taifa mbele na sio vijana kuwa watu wa kulalamika mitaani .

Misafi ambae amepata kuwa katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Makorongoni alisema kuwa jitihada kubwa zimekuwa zikifanywa na Rais Dkt Magufuli katika kuwaletea maendelea watanzani tena kwa kuwajali wanyonge zaidi .

Lakini wapo baadhi ya vijana ambao wao mbali ya kuwa na fursa za kuondokana na hali ya umasikini ama kati ya makundi ya watu wanaolalamika hali bila kufanya kazi ila vijana hao wamekuwa mbele kuongoza makundi ya wanaolalamika jambo mbalo si sahihi .

" Rais wetu Dkt Magufuli amekuwa mbele sana kulipeleka Taifa kwenye uchumi wa kati kwa kujenga miradi mbali mbali ya kiuchumi nchini tumeona miradi ya umeme ,Hospitali kila wilaya ,barabara ,maji ,,ununuzi wa ndege ,mashule na miradi mbali mbali mikubwa ambayo yote kwa ajili ya watanzania ila vijana badala ya kuibua miradi yetu wenyewe tumebaki kulalamika mitaani si sawa na hatumtendei haki Rais na serikali yetu " alisema

Jukumu kubwa la vijana ni kuungana pamoja na kufanya kazi zenye tija na pale ambapo unahitajika msadaa ama nguvu kutoka serikalini kuweza kutumia vikundi vya vijana walioungana pamoja kuomba serikali kuongeza nguvu na sio kushinda kulalamika pasipo kuwa na shughuli za kufanya .

Akitolea mfano alisema kwa upande wake ni kijana kama vijana wengine ambao wamekulia ndani ya chama na kufanya kazi za chama ila pamoja na kukitumikia chama sasa ameweza kujiongeza na kutafuta mtaji wake wa kununua mabasi zaidi ya moja na kuamua kufanya kazi ya usafirishaji .

Misafi alisema mbali ya kuwa amehama mkoa wa Iringa na kuhamia mkoani Dodoma kwa shughuli zake za kibiashara ila bado anaendelea kuwakumbuka vijana wa mkoa wa Iringa kata hiyo ya Makorongoni ambao walitokea kumwamini na kumchagua kuwa katibu mwenezi wa CCM wakati akiwa mgeni kutoka wilaya ya Imalinyi mkoani Morogoro ambako ndiko alikozaliwa .

Alisema amelazimika kuendelea kuwajali vijana hao kwa kuwa anatekeleza ilani ya CCM na alipata kuwaahidi kuwasaidia na anatarajia kuwatafutia mradi wa kiuchumi wa kufanya utakaowaingizia pesa vijana wa Makorongoni .

Kwa upande wake katibu kata wa CCM kata ya Makorongoni Jonhson Dick pamoja na kupongeza msaada wa Misafi kwa vijana hao bado alisema vijana wanaowajibu wa kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya CCM kwa kuhakikisha wanashiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2020 kwa kuchagua viongozi wanaofanana na Rais Dkt Magufuli.
Mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya Misafi ,George Misafi (kushoto) akimkabidhi mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) kata ya Makorongoni mjini Iringa Steven Chaula msaada wa shilingi 500,000 kwa ajili ya kununua vifaa vya vijana (picha na Francis Godwin)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...