Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mbwana Samatta na Mshambuliaji, Saimon Msuva rasmi wametua nchini kujiunga na timu hiyo kwa ajili ya mchezo wakuwania kufuzu Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON 2021) dhidi ya Equatorial Guinea, mashindano yatakayofanyika nchini Cameroon.

Samatta na Msuva watawaongoza wenzao 27 wa Kikosi cha Stars kwenye mchezo huo wa kwanza wa Kundi J utakaopigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Novemba 15 mwaka huu.

Baada yakutua nchini akitokea kwenye majukumu ya Klabu yake ya KRC Genk, Samatta amesema kama Nahodha hafahamu chochote kuhusu Guinea ya Ikweta, amesema hawezi kuzungumzia wao, amesema wataandaa kikosi kipindi hiki cha wiki moja kuhakikisha wanaimaliza Guinea katika mchezo huo.

"Nakumbuka mwaka juzi, katika michezo yakufuzu AFCON, tulicheza na Lesotho mchezo wetu wa kwanza lakini tulitoka sare ya 1-1, kitu ambacho tulijutia sana sisi kama timu wakati tulikuwa nyumbani", amesema Samatta.

Samatta amesema Taifa Stars itaandaa Kikosi vizuri ili kuhakikisha inapata ushindi katika mchezo wa kwanza, amesema kwa upande wake yupo vizuri kuwavaa Guinea ya Ikweta pamoja na Msuva.

"Miaka michache ijayo natamani kuona Wachezaji hata 8 tunacheza Ulaya ili wote tuje kuitumikia Timu ya Taifa, Watanzania watambue wanapokuja Uwanjani watambue kuwa wao ni Mchezaji wa 12, waje kwa wingi kuhakikisha timu yao inapata ushindi katika mchezo huo", amesema Samatta.

Kwa upande wake, Saimon Msuva amewaomba Watanzania kufika kwa wingi Uwanjani siku hiyo ya Novemba 15 kuishangilia Taifa Stars ili iweze kupata ushindi wake katika mchezo wake wa kwanza, amesema Tanzania tunahitaji kusonga mbele kisoka.

"Tumejiandaa vya kutosha katika Kikosi chetu chini ya Kocha Mkuu, Ndayiragije kilichobaki kufanya kazi hiyo Novemba 15 tukisaidiana na wenzetu waliotangulia kujiunga na Kikosi", amesema Msuva.

Wachezaji watakaoivaa Equatorial Guinea, Novemba 15 ni Mshambuliaji wa Genk Mbwana Samatta, Mshambuliaji wa Difaa El Jadida ya nchini Morocco Simon Msuva, Kiungo wa Tenerrife ya Hispania Farid Mussa. Beki wa Kulia wa Nkana ya nchini Zambia Hassan Kessy , David Kisu (Gor Mahia )na Eliuter Mpepo kutoka Buildcon Zambia.

Magolikpa Juma Kaseja (KMC), Metacha Mnata (Yanga) na mabeki ni Salum Kimenya (TZ Prisons), Mohamed Hussein (Simba), Gadriel Michael (Simba), Erasto Nyoni (Simba)Bakari Nondo (Coastal Union), Kelvin Yondani (Yanga), Dickson Job (Mtibwa).

Viungo ni Jonas Mkude (Simba), Abdul Aziz Makame (Yanga), Iddi Suleimani (Azam), Salum Abubakar (Azam),  Mzamiru Yassin (Simba), Frank Domayo (Azam), Miraji Athuman (Simba), Hassan Dilunga (Simba).

Kwa upande wa safu ya Usambuliaji ni Ditram Nchimbi (Polisi TZ), Shaban Iddi (Azam),Kelvin John ( Football House) na Ayoub Lyanga (Coastal Union).

Mchambuzi mahiri wa soka nchini Dkt Likky Abdallah akiwalaki Mbwana Samatta na Saimon Msuva Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...