Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MAADHIMISHO ya siku ya Takwimu Afrika yanayofanyika kila tarehe 18 Novemba kila mwaka yataadhimishwa tena mwaka huu yakiwa na malengo ya kuelimisha umma kote barani Afrika kuhusiana na umuhimu wa takwimu na kuongeza ufahamu juu ya nafasi na mchango wa tasnia ya takwimu na kuongeza ufahamu kuhusu nafasi na mchango wa tasnia ya takwimu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii barani Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Takwimu nchini (NBS) imeeleza kuwa Tanzania itaadhimisha siku ya takwmu ikiwa mwanachama wa Umoja wa Afrika na kila mwaka huungana na wanachama wengine wa umoja huo kuadhidhimisha siku hiyo kwa kufanya shughuli mbalimbali ambazo zinaakisi maudhui ya maadhimisho hayo na miongoni mwa matukio yatakayoambatana na maadhimisho hayo ni pamoja na mashindano ya kuandika Isha kwa wanafunzi wa shule za sekondari kote nchini.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa lengo la kuweka shindano hilo ni kuongeza ufahamu kwa vijana kuhusu masuala ya kitakwimu ikiwemo umuhimu na matumizi ya takwimu katika maendeleo pamoja na kuwahamasisha vijana kupenda tasnia ya takwimu amayo ni moja ya tasnia ambayo itawasaidia nakuwawezesha kutimiza ndoto zao za maisha.

Wanafunzi wa shule za Sekondari wameshauriwa kuandika insha kuhusiana na  Mada ya 'UMUHIMU WA TAKWIMU KATIKA KUPANGA NA
KUIMARISHA ELIMU YA SEKONDARI NCHINI TANZANIA' na urefu wa Insha usizidi maneno mia tano huku tarehe ya mwisho ya kuwasilisha insha hizo ikiwa ni Novemba 21 mwaka huu saa kumi kamili jioni na washindi watatangazwa na kupatiwa zawadi zao siku ya kilele cha siku ya maadhimisho ya siku ya Takwimu Afrika yatakayofanyika tarehe 28 Novemba, 2019 katika ukumbi wa mikutano wa Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Julius Nyerere kilichopo Mtaa waShaaban Robert jijini Dar es Salaam.
 Insha zote ziwasilishwe   kwa anuani zifuatazo:
Ofisi ya Taifa ya Takwimu,
Barabara ya Jakaya Kikwete,
S.L.P 2683,
DODOMA
AU
Ofisi za Takwimu za Mkoa ulipo
AU
Emails: sg@nbs.go.tz na nakala kwa joel.weja@nbs.go.tz, said.ameir@nbs.go.tz.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...