ASASI ya Tanzania Election Alliance(TanEA) imesema kuwa ili wananchi 
wadhihirishe utashi wao katika chaguzi ni dhahiri chaguzi lazima ziwe huru, haki,  wazi, sawa na za kuaminika huku ikisisitiza wapiga   kura wanapaswa kupiga kura bila woga, hofu au kuingiliwa  kusiko stahili. 

Hayo yamesemwa leo Desemba 2,2019 jijini Dar es Salaam na Wallance 
Mayunga wakati akizungumza na waandhsi wa habari walipokuwa wakitoa 
tathimini yao ya uchaguz ii wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 24,2019.

Amefafanua chaguzi ni michakato, ambayo idadi kubwa ya watu inachagua watu wachache miongoni mwao ili wawakilishe na kufanya maamuzi kwa niaba yao katika nafasi za kuchaguliwa au nafasi za kisiasa kupitia uchaguzi. Kupitia uchaguzi mtu anapewa nafasi ya kutenda kwa niaba ya wengine. 

"Hili hufanyika kwa kupiga kura, katika chaguzi za kisiasa, raia huamua nani awawakilishe katika nafasi ya Urais, Udiwani na kadhalika.Chaguzi za 
kidemokrasia zinamanisha wananchi sio tu wanapata fursa za kuchagua, bali pia mazingira yanayo faa kuchagua kwa uhuru, haki, uwazi na usawa,"amesema Mayunga.

Amefafanua ili kampeni ziwe huru na zenye utulivu wagombea na vyama vya siasa vinavyo shiriki kwenye uchaguzi havitawaliwi na vitisho au rushwa na mwamba wagombea wanafuata taratibu na mwenendo  katika kuendesha kampeni zao na kufuata kanuni za maadili zinazo ongoza mchakato wa uchaguzi.

"Vyama na wagombea wanaoshindana wanapatiwa fursa sawa za kusikilizwa.Pia vyama na wagombea wanao shindana wanapatiwa fursa sawa za kusambaza ujumbe wao kupitia vyombo vya habari na njia nyinginezo, zinazo kubalika katika kuwafikia Watanzania,"amesema.

Akifafanua zaidi kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019, amesema kuwa TanEA ilifanya uangalizi katika mikoa 13 ya Tanzania Bara na wilaya zipatazo 40 na jumla ya Watazamaji 150 walisambazwa katika Wilaya na Mikoa hiyo." TanEA inatumia fursa hii kuwapongeza Watanzania wote kwa kuwa na utaratibu wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Siyo nchi zote duniani wanayo nafasi hii.

"TanEA inavipongeza vyombo vya habari kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na asasi za kiraia katika  kuelimisha na kuhamasisha umma kujitokeza na kushiriki katika uchaguzi huu,"amesema Mayunga.


Hata hivyo TanEA wanatoa mapendetunatoa mapendekezo kadhaa kwa Serikali yakiwamo ya kushauri Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ufanyike sanjari na uchaguzi mkuu, kwa vile imedhihirisha hamasa katika uchaguzi wa Serikali za mitaani ndogo ukilinganisha na uchaguzi Mkuu unaochagua Rais, Wabunge na Madiwani.

" Ikiwezekana hili lifanyiwe kazi katika uchaguzi ujao wa 2025 mara baada ya uchaguzi mkuu wa 2020. Wananchi wengi wanadhani uchaguzi wa Serikali Mitaa hauna umuhimu. Ikifanyika hivi pia itapunguza gharama za uchaguzi kwa Watanzania, ambao ndio walipa kodi,"amesema Mayunga.

Pia wamependekeza vibali vya kutoa elimu ya mpiga kura, uraia na 
utazamaji/uangalizi wa uchaguzi vitolewe mapema. "Kwa mfano, mwezi Januari ili kutoa fursa kwa AZAKI na Taasisi mbalimbali kujiandaa kupata rasilimali na kupanga programu husika,".

Ameongeza mapendekezo mengine ni kwamba Asasi za Kiraia zishiriki 
kikamilifu katika kutoa elimu ya Mpiga kura na vile vile kushiriki kikamilifu 
katika uangalizi ili kuishauri Serikali kuboresha mazingira ya uchaguzi ikiwemo kasoro na dosari zinazojitokeza. 

Pia wanatoa mwito kwa AZAKI kushirikiana katika masuala haya muhimu ya Elimu ya Mpiga kura na uangalizi wa uchaguzi.Vyombo vya habari vinapaswa viendelee kushiriki kikamilifu pia kuelimisha wananchi, kusambaza taarifa sahihi kuhusu masuala ya uchaguzi na mchakato wa uchaguzi, tunavishauri vyombo vya habari vitimize wajibu wake ipasavyo.

"Tunaiomba Serikali ikae pamoja na makundi mbalimbali ya wadau wa uchaguzi kama vile AZAKI, vyama vya siasa, taasisi mbalimbali kufanya tathmini ya kungalia dosari zilizo jitokeza katika uchaguzi huu wa serikali za Mitaa uliopita na kuzifanyia kazi ili kuufanya uchaguzi ujao uwe huru, haki na usawa. 

"Pia vyama vya Siasa vishirikiane na serikali katika kuboresha mazingira ya uchaguzi. Serikali iendelee kutunza Demokrasia hapa nchini ili wananchi waweze kushiriki kikamilifu katika michakato ya uchaguzi na chaguzi,"amesema Mayunga.

Pamoja na mambo mengine amesema uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 nchini Tanzania si wa kawaida ukilinganisha na chaguzi nane zilizopita.Pia ni bora viongozi na wanachama na vyama hivyo na zaidi kujiepusha na hotuba zenye chembe chembe za kwenda kinyume cha sheria na utawala bora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...