Baadhi ya bidhaa za mafuta ya Parachichi yaliyozalishwa kwaajili ya matumizi ya kawaida ya Avomeru yanayotengenezwa na Jesse Oljange.
Mwanzilishi wa wa Kampuni ya Avomeru Group LTD, Jesse Oljange akizungumza na Michuzi Blog katika maonesho ya nne ya bidhaa za viwanda yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya JK. Nyere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

TATIZO la tunda la parachichi kuharibika limepungua kwa wakazi wa Arusha kwani mbunifu Jesse Oljange ameweza kubuni Mashine ya kutengeneza mafuta ya parachichi na kupelekea thamani parachichi kuongezeka.

Akizungumza na michuzi blog, Jesse Oljange amesema kuwa katika kuhakikisha matunda aina ya parachichi hayapotei bure ameweza kununua matunda hayo kwa wingi kwaajili ya kutengeneza mafuta. 

"Kwa sasa tunda aina ya parachichi haliharibiki hovyo, wala halidharauliwi kama zamani saivi parachichi ni tunda mhimu, na maisha yake yameongezeka kutoka siku tatu hadi kufikia miezi tisa hadi miezi 12". Amesema  Oljange.

Oljange amesema ameweza kushirkiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) katika kutatua changamoto mbalimbali za kijamii alivyoweza kutumia ubunifu wake na kuweza kutengeneza Mafuta ya parachichi halisi (Avomero oil).

Amesema parachichi zilikuwa zinaharibika ila kwa sasa wananchi wamepata soko la kuuzia parachichi hizo na kujipatia kipato.

"Wale wakulima wadogo walikua wanauza debe la parachichi ambalo ni sawa na parachichi 70  kwa shilingi elfu mbili sasa wananchi hao wanauza  parachichi 42 kwa shilingi elfu nane". 

Jesse amesema kuwa mpaka sasa parachichi katika eneo hilo ambapo ameweka kiwanda kidogo limekuwa na thamani kubwa kuliko ilivyokuwa mwanzo.

Hata hivyo Jesse amesema kiwango kikubwa ameweza kusaidia jamii kupinguza uzito wa kusafirisha parachichi na kuweza kusafirisha mafuta ambayo yanatumika kwa matumizi mengi.

Hata hivyo amewashukuru Tume ya Sayansi na Teknolojia kwa kuwawezesha na kupokea wazo lao kwani mpaka sasa mafuta ya Avomeru yanauzwa hadi nje ya nchi.

Hata hivyo Oljange amewakaribisha wananchi katika viwanja vya sabasaba kwaajili ya kuwaunga mkono pamoja na kwenda kuona ubunifu walioufanya katika kulipathamani Parachichi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...