Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Jana Usiku Desemba 07 imeandikwa tena Historia kwa wapenzi wa Burudani ndani ya Manispaa ya Bukoba na Viunga vyake, katika Tamasha kubwa linaloandaliwa na Kituo cha Redio Kasibante Fm, kilichopo Mkoani Kagera, ambalo hufanyika Desemba kila Mwaka, ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kuanzishwa kwa kituo hicho.

Burudani hiyo ya kiwango cha aina yake imefanyika ndani ya Kumbi za Lina's Night Club kwa kuwakutanisha mamia ya wapenzi wa Burudani hususani wasikilizaji wa kituo hicho pendwa, pamoja na wasanii nguli wa muziki wa Dansi na Bongo Fravoul.

Burudani ilianza majira ya saa tatu usiku kwa kutanguliwa na wasanii wa nyumbani (wenyeji) akiwemo msanii anaefanya vizuri katika kiwanda cha Bongo fravoul HarmyD planet, na kisha baadae kutoka Jijini Dar es salaam orodha ilifunguliwa na Baddest 47 mzee wa nikagongee.

Katika kuhakikisha kila aliyefika ukumbini pale anapata burudani aliyostahili, Mzee wa Kitambaa cheupe King Kikii alionesha umahiri wake na kudhihirisha kuwa Ng'ombe hazeeki maini pale alipowakumbusha wapenzi wake Kitambaa cheupe.

Shangwe zilidishwa na kunogeshwa zaidi na Baba na mwana Nguza Viking na Papii Kocha, walioonekana kuuteka usiku wa burudani kwa kuwanyanyua mamia ya wakazi wa Kagera kwenye viti vyao na kuimba nao nyimbo zao zilizowahi kutamba Salima, Fanta, Sea na nyingine. 

Mwisho Marioo kutoka sekta ya  Bongo fravoul akafunga kazi kwa kubembelezana na wadau wake kupitia ngoma zake kalii ikiwa ni hitimisho la burudani hiyo ya kumbukizi ya kuanzishwa kwa matangazo ya kituo hicho cha Redio mnamo Tarehe 07, Desemba 2008 ikiwa imetimiza miaka 11 sasa mlangoni kwako.


Pichani ni Papii Kocha mtoto wa Mfalme akizidi kuwateka mashabiki waliofurika katika usiku wa Kasibante Festival 2019 katika viwanja vya Lina's kwa burudani muruwaa.

Pichani Ni mzee wa Kitambaa Cheupe Nguza Viking akichungulisha mashabiki kwa staili yake ya "Chunguliaaa"

Pichani Marioo akiendelea kusuuza nafsi za mashabiki kwa kukonga nyoyo zao na ngoma zake kalii ikiwemo "INATOSHA"

Pichani ni mashabiki wakiendelea kuchukua kumbukumbu katika simu zao pamoja na Msanii Baddest 47 baada ya kugongewa Banana
Mashabiki wakiendelea kuserebuka ukumbini humo

Mmoja wa wapenzi wa Muziki akimtunza Mkongwe wa Muziki Mzee Nguza kwa namna anavyomudu kulicharaza gitaa na kuimba kwa wakati mmoja.
Mzee Nguza pamoja na kubarikiwa sauti ya kuimba pia ni hodari wa Gitaa, kama anayoonekana akicharaza gitaa la solo akimpa tafu mwanae kwenye ngoma ya Sea


Pichani wanaoneka vibonge Staff wa Kasibante FM wakiongozwa na Madame Abella Mkurugenzi Mtendaji wa Kasibante FM wakiangusha moja moja jukwaani pale Fanta ya Papii Kocha ilipokuwa ikirindima.
Burudani ikiendelea kutolewa ukumbini humo
Wapenzi wa Muziki wa Dansi wakiendelea kujimwaya mwaya ukumbini

.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...