Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Kigoma

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) umesema unatekeleza miradi 27 yenye thamani ya Sh.bilioni 123.345 katika Bandari za Ziwa Tanganyika ukiwa ni uwekezaji mkubwa kupata kutokea nchini katika ukanda huo wa ziwa hilo.

Hayo yameelezwa na Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika Percival Salama wakati akizungumza na waandishi wa habari walioko kwenye ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya uboreshaji wa miundombinu katika bandari za maziwa makuu unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari(TPA).

Akizungumza zaidi kuhusu miradi hiyo na hasa kwa kuanza na Mkoa wa Kigoma  Salama amesema kiwango hicho cha fedha ambacho kimewekwa katika kutekeleza miradi hiyo katika Bandari za Ziwa Tanganyika kinaonesha dhahiri dhamira njema ya Serikali ya Awamu ya Tano kusogeza huduma za bandari karibu na wananchi na kubwa zaidi TPA inatambua umuhimu wa miundombinu ya bandari iliyoboreshwa katika maeneo yote yenye maziwa makuu.

Amesema kwa upande wa Mkoa wa Kigoma wameendelea kutekeleza miradi ya kimkakati ambapo amefafanua kuna mradi mkubwa unaondelea ukiwemo wa kujenga miuombinu ya bandari ya Kibirizi, Bandari ya Ujiji pamoja na ofisi mpya ya Meneja wa Bandari.

"Mradi huu unatekelezwa na mkandarasi CR15G China Ralway Cooperation na ndio tumeingia naye mkataba wa miezi 24 na ameanza kazi Machi 5, mwaka 2019, mradi huu una gharama ya Shilingi bilioni 32. 525.Ni uwekezaji mkubwa ambao unakwenda kubadili mazingira na muonekano mpya wa bandari kwenye Mkoa wa Kigom,  kwa hiyo Bandari ya Kibirizi tunajenga gati ya urefu wa mita 250.

"Pia tunajenga mashed matatu makubwa, eneo la kupumzikia abiria, ofisi na miundombinu mengine wezeshi ambayo itafanya bandari hii ya majahazi kuwa nzuri na inayoweza kutoa huduma zinazotakiwa. Lakini tuna jengo la Meneja wa Bandari amba;o ujenzi wake tayari umeanza , ni jengo zuri bora na ramani yake ni nzuri ambayo nayo  ipo ndani ya mradi wa Kibirizi,"amesema.

Ameongeza kuwa Bandari ya Ujiji wanatengeneza gati ya urefu wa mita 110 na kwamba Ujiji ni mji wa kihistoria ambako katika bandari hiyo wanajenga miundombinu ikiwemo eneo la chakula, sehemu ya kupumzikia abiria, maghala ya mizigo na kwamba huo ni mradi mmmoja ambao unatekelezwa ndani ya Mkoa wa Kigoma.
 
"Mradi wa pili ambao unatekelezwa na wakandarasi wawili kwa wakati mmoja Satellite pamoja na Josam ni mradi wa ujenzi wa Bandari Kavu ya Katosho ni mradi mkubwa wa Sh bilioni 2.9 unatekelezwa kwa muda wa miezi tisa na sasa hivi wako karibu asilimia 80 ya utekelezaji.Kimsingi tunatarajia ifikapo Desemba 27, mwaka 2019 wakatabidhi mradi na kwa kasi ambayo wanakwenda nayo tunaamini kabisa kufika tarehe hiyo  wataukabidhi kwani ulianza kutekelezwa Machi 28,2019, kwa hiyo utaona tulianza  kwa kusuasua lakini kuanzia Agosti ulikuwa asilimia 10 ya utekelezaji ambapo hadi sasa wamefanya kazi kwa asilimia 70.

"Pia katika Mkoa wa Kigoma tuna eneo la Kagunga ambalo kwa sasa hili ni eneo la kipekee kwa sababu pale TPA imefanya utekelezaji wa miradi mitatu kwenye eneo moja.Hii ni bahati kubwa kwa Kigoma Vijijini kupata mradi wa namna hiyo na pale Serikali kupitia Mamlaka imewekeza karibu Sh.bilioni 4. 09, unazungumzia mradi wa Soko la Kagunga la Sh.milioni 190, mradi wa barabara wa mita 700 wa Sh.milioni 553, mradi wa gati la Kagunga wa Sh bilioni.5. 357,"amesema.

Ameongeza kuwa  kutokana na uwepo wa mradi huo wananchi wanatakiwa kufahamu pale kuna soko la kimataifa ambalo limelenga kuwaleta karibu DRC pamoja na Burundi hasa kwa kuzingatia pale ni mpakani mwa Burundi na Tanzania.Pia  kwa maji ni mpaka na DRC, kwa hiyo sasa watu watakusanyika kufanya biashara kwenye eneo hilo.

"Kwa tafsiri yetu wananchi wa Tanzania na Burundi watafanya biashara ya kuuza mazao yao na mnajua wenzetu wa DRC wanatumia rasilimali yao fedha kufanyabishara ya kununua bidhaa kutoka Tanzania lile ni eneo moja wapo ambalo litavutia wafanyabishara wengi kwenda kufanyabishara kwenye lile eneo.

"Na ile Bandari ya Kagunga kwa sasa imekamilika kwa asilimia 100, sisi TPA tumeshaanza kufanyakazi tangu Desemba 12,mwaka 2019, tayari na wafanyakazi wapo pale.Nataka niwaambie wana Kagunga na Kigoma kwa ujumla kwamba sasa Bandari yetu ya Kagunga imeanza kufanyakazi,"amesema.

Salama amewashauri wenye boti za abiria wapite katika bandari hiyo na kwamba watu kutoka Burundi na DRC nao wapite hapo na hata wa kutoka Zambia pitieni hapo kwani watapata huduma kwenye  gati na miundombinu mizuri iliyowekezwa na Serikali kupitia TPA na hayo ndio mapinduzi ya uboreshaji na uwekezaji wa huduma unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli kupitia TPA chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. 
 Boti za abiria zikiwa zimeegeshwa katika Bandari ya Kibirizi katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma
 Mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi ya Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika ukiendelea katika eneo la Bandari ya Kigoma.
 Mmoja wa wananchi wa Kigoma Mjini akitoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Tano na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) kutokana na hatua iliyochukua ya kuboresha miuomdombinu ha bandari ya Kibirizi na hasa ujenzi wa gati.
 Baadhi ya mizigo ikionekana katika bandari ya Kibirizi mkoani Kigoma ikisubiri kusafirishwa kutoka bandari hapo kuelekea nchini jirani za Burundi na DRC.Bandari ya Kibirizi ni moja ya bandari ambayo imetengewa fedha kwa ajili ya kuboreshwa kwa miundombinu yake.
 Baadhi ya magari yakiwa yamebeba mifuko ya saruji katika Bandari ya Kibirizi ambayo inasubiri kupakiliwa na kisha kuingizwa kwenye meli ili kusafirishwa katika nchi jirani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...