Issa Mtuwa – “WM” Nzega

Waziri wa Madini Doto Biteko amesema ataendelea kuongea kwa namba (takwimu) badala ya maneno huku akitamba kuwa wizara yake itavuka malengo ya makadirio ya makusanyo ya fedha zilizopangiwa na wizara yake kukusanya ambayo ni bilioni 475 katika mwaka wa 2019/20 huku akibainisha kuuwa ndani ya miezi 5 tu teyari wizara yake imeshakusanya bilioni 205.

Ameyasema hayo leo tarehe 7/12/2019 Wilayani Nzega alikokwenda kukabidhi Leseni 11 kwa vikundi 10 vya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu. Ameongeza kuwa kuongea ongea hakusaidii zaidi ya kufanya kazi na ukifanya kazi acha namba zikusaidie kueleza unachokifanya.

Pamoja na kukabidhi leseni hizo, Biteko ametoa masherti kwenye eneo moja la uchimbaji aliloliwekea mashaka kuhusu usalama wake kutokana na hali yake huku akiagiza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya chini ya mwenyekiti wake ambae pia ni Mkuu wa Wilaya Godfrey Ngupula kuhakikisha utaratibu wa usalama umezingatiwa kabla ya kuanza kuchimba.

Vikundi vilivyokabidhiwa leseni hizo ni pamoja na; Msilale Miners Group, Jimbo la Nzega Vijijini, Undomo Miners Group, Hapa Kwetu Group, Umoja wa Wachimbaji Mwanshina, Mkombozi Mining Group, Imalamakoye Miners Group, Salama Miners, Makalanga Minerals Group na Nzega Miners Association.

Biteko amesema uthubutu wake na viongozi wenzake wa wizara nzima ndio unaopelekea kuiweka sekta ya madini kwenye mwendo “mdundo” huku akiahidi yeyote anayetaka kurudisha nyuma mwendo huo hatokubaliana nae.

Ameongeza kuwa, mara kwa mara halali usiku kwa ajili ya kupokea simu za wananchi wakimpa taarifa za utoroshaji wa madini na taarifa mbalimbali. Hata hivyo amesema anakerwa na vitendo vya uchonganishi kwa kutoa taarifa za uongo huku akiwaomba wananchi kutoa taarifaa zenye ukweli na usahihi ili kulisaidia tafia.

“Madini haya si yangu mimi wala ya Rais John Pombe Magufuli, ni madini ya Watanzania na sote tunawajibu wa kuyalinda, kazi yangu ni kusimamia maekezo ninayopewa na Mhe. Rais na kuhakikisha sekta hii inachangia kwenye pato la taifa kama inavyostahili. Narudia tena, anae stahili sifa katika haya yote yanayofanyika kwenye madini sio Mimi Doto Biteko, anaye stahili sifa na pongezi zote ni Rais John Pombe Magufuli kwani yeye ndiye anaye elekeza na mimi ni msimamizi tuu wa kutekeleza yale anayo yaagiza.”. Alisema Biteko.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Leseni kutoka Tume ya Madini Mhandisi Yahaya Semamba amewaambia wanavikundi waliopatiwa leseni kuwa pamoja na kupatiwa leseni hizo wanapaswa kuzingati masherti ya leseni hizo na kwamba watakao kiuka watawafutia leseni yao. Miongoni mwa masherti hayo ni kuhakikisha ulipaji wa maduhuli ya serikali, kutunza mazingira, kuzingatia usalama na masherti mengine yote.

Akiongea kwa niaba ya wanavikundi wenzake waliokabidhiwa leseni Aluna Mgalula amemshukuru Waziri wa Madini na Mkuu wa Wilaya kwa kuwaondelea kero yao ya kupatiwa leseni. Ametoa ushuhuda wa namna alivyokuwa anamsumbua waziri Biteko kwa kumpigia simu hata usiku wa manane huku akipokea na kumsikiliza.

Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wilayani Nzega ametoa pongezi kwa serikali na wizara ya madini huku akimshukuru waziri Biteko kwa namna anavyo wasaidia wachimbaji wadogo katika kuwapatia maeneo mbalimbali na kuwafanya wachimbaji kuwa na utulivu katika kazi zao.
Waziri wa Madini Doto Biteko akikabidhi Leseni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu kwa mmoja wa mwakilishi wa moja kati ya vikundi 10 vilivyo kabidhiwa leseni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...