Mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 25 ya Huduma ya Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC), Baba Askofu mstaafu wa Kanisa la Tanzania  Evangelist Assemblies of God ( EAGT) Dkt. Asumwisye Mwaisabila (kushoto),akiongoza kumuombea Askofu wa Kanisa hilo, Flaston Ndabila na mke wake Janeth katika maadhimisho hayo yaliyofanyika jana.
Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC hapa nchini, Flaston Ndabila na mke wake Janeth wakiingia kanisani katika maadhimisho hayo. Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC hapa nchini, Flaston Ndabila na mke wake Janeth wakiwapungia mikono waumini wa kanisa hilo wakati wakiingia kanisani katika maadhimisho hayo.
 Watoto wakiwa katika maadhimisho hayo.
 Maadhimisho yakiendelea.
 Watumishi wa Mungu kutoka nje ya nchi wakionesha mshikamano kwenye maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Bishop Musa Ngobese (Afrika Kusini), Bishop Mark Mugekenyi (Kenya) na Mchungaji Hererimana Tharcise kutoka Burundi .
 Nyimbo zikiimbwa.
 Maadhimisho yakiendelea.
 Maadhimisho yakiendelea.
 Maadhimisho yakiendelea.
 Nyimbo zikiimbwa.
 Mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 25 ya Huduma ya Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC), Baba Askofu mstaafu wa Kanisa la Tanzania  Evangelist Assemblies of God ( EAGT) Dkt. Asumwisye Mwaisabila akiingia kanisani.
 Watoto wa Askofu Ndabila wakiingia kanisani.Kutoka kushoto  ni  Rehema, Tabitha na kaka yao Gadi.
 Mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 25 ya Huduma ya Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC), Baba Askofu mstaafu wa Kanisa la Tanzania  Evangelist Assemblies of God ( EAGT) Dkt. Asumwisye Mwaisabila akiwa na Mchungaji Dkt.Nicku Kyungu kutoka Huduma ya Igo Africa for Jesus Prayer Ovement (Marekani)
 Maadhimisho yakiendelea.
 Maadhimisho yakiendelea.
 Katibu Mstaafu wa CPCT Taifa, Askofu  Dkt. David Mwasota, akiomba kabla ya kuanza kwa maadhimisho hayo.
 Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC hapa nchini, Flaston Ndabila, akitoa historia fupi ya kanisa hilo.
 Watoto wa Askofu Ndabila wakiwa katika maadhimisho hayo.Kutoka kushoto  ni  Gadi, Rehema na Tabitha.
 Katibu wa Askofu Mkuu wa Makanisani ya ABC hapa nchini, Peter Sifi akitoa taarifa ya kanisa hilo.
 Mchungaji Dkt.Nicku Kyungu kutoka Huduma ya Igo  Africa for Jesus Prayer Ovement (Marekani), akiomba katika maadhimisho hayo.
 Bibi na Bwana Dickson Malali wakizungumzia kanisa hilo.
 Bwana na Bibi, Martin Milyango wakizungumzia kanisa hilo.
 Bwana na Bibi, Martin Milyango wakikabidhi zawadi.
 Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC hapa nchini, Flaston Ndabila na mke wake Janeth wakipokea zawadi ya mashine ya kufulia.
 Bwana na Bibi, Martin Muhembano wakizungumzia kanisa hilo.
 Pastor Florian Katunzi  na mke wake Rachel wakizungumza.
 Bishop Musa Ngobese kutoka Afrika Kusini, akizungumza
 Bishop Mark Mugekenyi,  akizungumza.
 Mchungaji Tharcise kutoka Burundi, akikabidhi zawadi.
 Askofu Dkt. Eric Mwabigaja, akikabidhi zawadi.
Mchungaji Dkt.Nicku Kyungu kutoka Huduma ya Igo Africa for Jesus Prayer Ovement (Marekani),akikabidhi zawadi.
 Zawadi ya vitenge ikienda kutolewa.
 Majirani wa kanisa hilo wakitoa zawadi ya jogoo.
 Majirani wa kanisa hilo, wakizungumza.
 Wanafamilia ya Askofu Ndabila katika picha ya pamoja.
 Keki ikikatwa.
 Watoto wakilishwa keki.
Mchungaji, Nathaniel Ndabila akifunga maadhimisho hayo kwa maombi.
Na Dotto Mwaibale
KANISA la Abundant Blessing Centre la Tabata Mandela jijini Dar es Salaam linatarajia kuwekeza katika miradi mbalimbali ili kuweza kusaidia jamii hasa vijana waweze kujikomboa kiuchumi.
Hayo yalielezwa jana katika hafla ya  maadhimisho ya miaka 25 ya huduma ya kanisa hilo wakati wa utoaji wa taarifa fupi iliyosomwa na Peter Sifi ambaye ni Katibu wa Askofu Mkuu wa Makanisani ya ABC hapa nchini, Flaston Ndabila.
"Katika kipindi hiki cha miaka 25 ya huduma ya kanisa letu tumefanya mengi lakini sasa tunataka kujikita katika uwekezaji wa kujenga chuo cha biblia ambacho ndani yake kutakuwa na chuo cha ufundi " alisema Sifi.
Alisema chuo hicho, kitatoa mafunzo ya ufundi washi, umeme, ushonaji, kompyuta, ujenzi, ushauri wa masuala ya ujasiriamali, useremala  na kuwa  tayari kanisa hilo limetenga sh.milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa kisasa  ambao ujenzi wake unatarajia kuanza hivi karibuni eneo la Kifuru Manispaa ya Ilala.
Alisema lengo la kuanzisha kwa uwekezaji huo ni kutoa fursa kwa wachungaji watakao kuwa wanasoma kwenye chuo hicho kujifunza stadi za kazi mbalimbali badala ya kutegemea uchungaji pekee na baada ya mafunzo hayo nao wapeleke elimu hiyo kwa jamii.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Baba Askofu mstaafu wa Kanisa la Tanzania  Evangelist Assemblies of God  (EAGT) Dkt.Asumwisye Mwaisabila ambaye ni miongoni mwa wazee wenye wanaoheshimiwa aliyedumu katika imani kwa muda mrefu akifanya kazi pamoja na Mzee Moses Kulola na Mungu amemjalia neema katika imani na usemi aliwataka wachungaji kufanya kazi ya utumishi kwa nguvu zote ili waje waweke alama ya utumishi wao.
"Kazi ya utumishi inahitaji uvumilivu na kujituma na sio mchezo mchezo mwenzetu Ndabila sasa anaadhimisha miaka 25 tangu aanze huduma hii na amepita katika magumu mengi na leo anamshukuru Mungu kwa kumfikisha hapa alipo mungu aendelee kumbariki zaidi huduma yake ikue zaidi ya hapo" alisema Mwaisabila.
Askofu Flaston Ndabila akitoa historia fupi ya kanisa hilo alisema yeye na mke wake walipita katika changamoto nyingi ikiwemo ya kulala njaa wakati wakianza huduma hiyo ya kichungaji huku wakiwa na mshirika mmoja tu kwa kipindi cha miaka miwili.
Alisema wanamshukuru mungu kwani hivi sasa wanawachungaji na baadhi ya makanisa yamejengwa na mengine yanaendelea kujengwa.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mchungaji Hererimana Tharcise kutoka Burundi alisema Tanzania ni nchi rafiki na nchi ya Burundi kwani ilijihirisha mwaka 2015 wakati lilipotokea jaribio la kutaka kumpindua Rais wa nchi hiyo wakati yupo hapa ambapo Tanzania ilisaidia kumrudisha nyumbani na mapinduzi hayo kushindwa.
Akimzungumzia Askofu Ndabila, Tharcise alisema mafunzo aliyompa yamemsaidia sana katika kanisa lake na yamebadilisha maisha yake ukilinganisha na hapo mwanzo.
Katika maadhimisho hayo maaskofu na wachungaji kutoka ndani na nje ya nchi walihudhuria baadhi yao ni Mchungaji Tharcise kutoka Burundi, Bishop Mark Mugekenyi (Kenya), Bishop Musa Ngobese (Afrika Kusini), Katibu Mstaafu wa CPCT Taifa, Askofu  Dkt. David Mwasota, Mchungaji Dkt. Nicku Kyungu kutoka Huduma ya Igo  Africa for Jesus Prayer Ovement (Marekani), Pastor Florian Katunzi na Askofu Primus Ishobeza na wengine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...